Fataawaa: Mukhtasari Wa Fataawaa Kuhusu Yanayobatilisha Na Yasiyobatilisha Swawm
Yafuatazo Ni Mukhtasari Wa Mas-alah Ambayo Aghlabu Huulizwa Khaswa Katika Ramadhwaan Kuhusiana Na Swawm
1-At-Tahaamiyl: (Suppository) Dawa Za Kuteremsha Homa Zinazowekwa Kwa Njia Ya Utupu Wa Nyuma
Hukmu Yake: Haibatilishi.
[Imaam ibn ‘Uthaymiyn]
2-Dawa Ya Macho Ya Maji (Eye Drops)
Hukmu Yake: Haibatilishi. Lakini atakapohisi ladha ya hiyo dawa kwenye koo lake, basi kiakiba akilipa hiyo siku ni bora.
[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn]
3-Wanja Wa Macho
Hukmu Yake: Haibatilishi na lakini ni bora atumie usiku baada ya kufuturu.
[Ibn ‘Uthaymiyn, Ibn Baaz]
4-Dawa Ya Kudondoshea Masikioni
Hukmu Yake: Haibatilishi.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
5-Kipulizo Cha Pumu.
Hukmu Yake: Haibatilishi.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn, Al-Lajnah Ad-Daaimah]
6-Kipulizo; Mashine Ya Kuvuta Hewa (Oxygen)
Hukmu Yake: Haibatilishi kwa kuhitajika kwa dharura.
[Ibn ‘Uthaymiyn]
7-Sindano Ya Penicillin
Hukmu Yake: Haibatilishi.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
8-Sindano Ya Insoline Kwa Mgonjwa Wa Kisukari
Hukmu Yake: Haibatilishi.
[Ibn ‘Uthaymiyn, Ibn Baaz]
9-Sindano Ya Ganzi Kwa Ajili Ya Kung’olewa Jino Na Kuweka Mjazo Wa Meno Na Kusafishwa Meno
Hukmu Yake: Haibatilishi. Lakini atahadhari kumeza chochote katika dawa na damu (kwa maana akimeza atabatilisha Swawm).
[Ibn Baaz]
10-Kutumia Manukato Mazuri Na Kuyanusa
Hukmu Yake: Haibatilishi.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
11-Kunusa Harufu Ya Udi Uliofukizwa
Hukmu Yake: Haibatilishi.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
12-Dawa Ya Kulainisha Mdomo (Lip Balm)
Hukmu Yake: Haibatilishi, kwa sharti kwamba asimeze kitu.
[Ibn ‘Uthaymiyn]
13-Vipodozi (Make Up)
Hukmu Yake: Haibatilishi.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
Tanbihi: Mwanamke hapaswi kujipamba kudhihirisha mapambo yake kwa wanaume ajnabiy wasio mahaarim wake.
14- Kuvuja Damu Pua Na Kun’goa Jino Huku Damu Ikitoka
Hukmu Yake: Haibatilishi.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
15-Kutolewa Damu Kwa Ajili Ya Kipimo
Hukmu Yake: Haibatilishi.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
16-Kuota Kitendo Cha Ndoa Na Kutokwa Manii
Hukmu Yake: Haibatilishi
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
17-Kutokwa Na Madhii. (Madhii Ni Maji Mepesi Mno Yenye Kunatanata Yanayotoka Wakati Wa Matamanio Ya Kimwili)
Hukmu Yake: Haibatilishi
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
18-Kuogelea Na Kupiga Mbizi
Hukmu Yake: Haibatilishi.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
19-Dawa Ya Kusukutua
Hukmu Yake: Haibatilishi kwa sharti kuwa asimeze kitu.
[Ibn ‘Uthaymiyn]
20-Kutumia Mswaki
Hukmu Yake: Haibatilishi.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
Lakini ni mswaki wa kawaida na si ambao una ladha.
21-Dawa Ya Kusafisha Meno
Hukmu Yake: Haibatilishi ikiwa haitomezwa ikaingia tumboni. Na lililo salama zaidi ni kutokuitumia kwa sababu ina nguvu kali.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
22-Kumeza Makohozi
Hukmu Yake: Haibatilishi ikiwa haitofikia mdomoni. Ama ikifikia mdomoni akameza, basi inabatilisha Swawm.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
23-Kuonja Chakula
Hukmu Yake: Haibatilishi lakini bila ya kumeza na wala asifanye mtu isipokuwa kwa dharura.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
24-Vidonge Vinavyoweka Chini Ya Ulimi Kwa Kutibu Maradhi Ya Moyo
Hukmu Yake: Haibatilishi ikiwa havitoyeyuka na kumezwa mate yake ambayo yameyeyuka ndani ya mdomo. Hakika vinabatilisha Swawm. Lakini vikiwa haviyeyuki na havimezwi, basi havina madhara.
[Ibn ‘Uthaymiyn]
25-Dawa Ya Kudondoshea Puani
Hukmu Yake: Inabatilisha ikifikia tumboni [akimeza].
[Ibn ‘Uthaymiyn]
Dawa ya pua haifai kwa mwenye Swawm na atakayetia ikafikia kooni akasikia ladha yake, basi alipe Swawm yake.
26-Viraka Vya Nikotini (Vya Kubandika Mikononi Au Mabegani Kusaidia Wavutaji Sigara Waache Uvutaji)
Hukmu Yake: Inabatilisha.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah]
27-Hijaamah (Kupigwa Chuku, Kuumikwa)
Hukmu Yake: Inabatilisha.
(Lakini Wanachuoni wengine wanaonelea ikiwa haitomdhoofisha anayefanyiwa Hijaamah, basi haibatilishi).
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
28-Kuchangia Damu
Hukmu Yake: Inabatilisha ikiwa ni nyingi (na kumdhoofisha mtoaji damu) kama vile kiasi cha damu ya Hijaamah.
[Ibn ‘Uthaymiyn]
29-Damu Inayotoka Katika Kidonda
Hukmu Yake: Inabatilisha ikiwa si kwa khiari yake kama vile kutolewa damu nyingi kwenye mishipa kwa ajili ya vipimo, lakini ikiwa ni kwa dharura bila ya khiari yake basi haibatilishi.
30-Kutapika Kwa Makusudi
Hukmu Yake: Inabatilisha ikiwa kwa makusudi. Ikiwa si makusudi haibatilishi.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
31-Sindano Ya Kuingiza Chakula Kupitia Maji Mwilini Kumtia Mtu Nguvu
Hukmu Yake: Inabatilisha.
Ama sindano ya misuli au ya mishipa au ya ngozi haibatilishi. Na ni salama zaidi kufanya usiku baada ya kufuturu.
[Ibn ‘Uthaymin, Ibn Baaz]
32-Kuvuta Harufu Ya Moshi Wa Udi
Hukmu Yake: Inabatilisha ikiwa anajua, ama ikiwa kunusa tu haibatilishi.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
33-Kujichua (Masturbation)
Hukmu Yake: Haijuzu katika Ramadhwaan wala nje ya Ramadhawaan na inabatilisha Swawm.
[Ibn Baaz, Ibn ‘Uthaymiyn]
34-Kudungwa Sindano
Hukmu Yake: Haibatilishi. Ama ikiwa ni kwa ajili ya kuingiza chakula au nguvu ya chakula (kama glucose) inabatilisha. Na usalama zaidi kutumia usiku [baada ya kufuturu].
[Ibn Baaz]
35-Kupaka Hinna
Hukmu Yake: Haibatilishi.
[Ibn ‘Uthaymiyn]
36-Kula Au Kunywa Kwa Kusahau
Hukmu Yake: Haibatilishi, lakini mtu anapokumbuka tu aachilie mbali hata kama kimo mdomoni akiteme.
[Ibn ‘Uthayimyn].
37-Kuvuta Sigara
Hukmu Yake: Inabatilisha na ni haramu wakati wowote katika Ramadhwaan na nje ya Ramadhwaan.
[‘Ibn ‘Uthaymiyn]
38-Kuoga
Hukmu Yake: Haibatilishi.
[Ibn ‘Uthaymiyn]
39-Kumeza Chakula Kilichokuja Kwa Kucheua
Hukmu Yake: Inabatilisha ikiwa chakula au maji aliyocheua yatafika mdomoni akameza, ama ikiwa yameishia kooni basi hana juu yake chochote
[Ibn ‘Uthaymiyn]
40-Kusafishwa Damu Ya Mafigo (Dialysis)
Hukmu Yake: Inabatilisha na inampasa alipe Swawm yake.
[Ibn Baaz]
41-Maongezi Maovu Ya Haramu
Hukmu Yake: Hayabatilishi lakini thawabu zitapunguka na kama yanahusiana na haki ya mtu (Kumtusi mtu), basi itampotezea kabisa thawabu za Swawm.
[Ibn Baaz]
42-Kumeza Mate
Hukmu Yake: Haibatilishi.
[Ibn Baaz]
43-Kumeza Maji Wakati Wa Wudhuu
Hukmu Yake: Haibatilishi ikiwa si kwa kukusudia.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah]