Pizza Ya Sosi Ya Zaytuni, Nyanya Za Kukausha Juani (Sun-Dried Tomatoes)

Pizza Ya Sosi Ya Zaytuni, Nyanya Za Kukausha Juani (Sun-Dried Tomatoes)

 

Vipimo Vya Unga:

 

Unga wa ngano - 3 Vikombe vya chai

Chumvi - 1 1/2 Kijiko cha chai

Sukari - 3/4 Kijiko cha chai

Maji - 1 3/4 Vikombe vya chai

Hamira - 1 Kijiko cha chai kilichojaa

Mafuta ya zaytuni - 4 Vijiko vya supu

 

 

Vipimi Vya Sosi

 

Kitunguu maji – 2 katakata

Nyanya/tungule 3 saga

Nyanya kopo

Nyanya kavu za juani (Sun-dried tomatoes) – kiasi robo kikombe

Zaytuni (olives) – 1 kikombe (zikate slesi)

Oregano – kijiko cha chai

Chumvi kiasi

Pilipili manga – 1 kijiko cha chai

Mafuta – 3 vijiko vya supu

 

Namna Ya Kutayarisha Unga:

 

  1. Changanya unga, pamoja na chumvi, sukari, na hamira, mafuta ya zaytuni katika machine ya kukandia.
  2. Tia maji kidogokidogo huku unachanganya mpaka  unga ukandike vizuri na ulainike.
  3. Ufunike na uache uumuke kwa masaa 2 au zaidi.
  4. Washa oveni moto wa 440F.

 

Namna Ya Kupika Sosi Na Pizza

 

  1. Katika sufuria tia mafuta, ukaange kitunguu na nyanya hadi viwe laini.
  2. Tia nyanya ulosaga au ukate ndogo ndogo, tia nyanya kopo, na tia oregano, pilipili manga. Tia sun-drid tomatoes ulokatakata slesi.
  3. Unga ukishauumuka, katakata vidonge ufunue kutandaza kidogo kisha pakaza sosi, na mwagia zaytuni.
  4. Paka mafuta katika treya uchome (Bake) pizza hadi ziive.
  5. Epua zikiwa tayari

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

Share