Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kujifunika Kichwa (Kuvaa Kofia Kilemba n.k) Katika Swalaah
Kujifunika Kichwa (Kuvaa Kofia Kilemba n.k) Katika Swalaah
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
“Kujifunika kichwa (kuvaa kofia, kilemba n.k) katika Swalaah ni khiari ya mtu kwa kuwa ‘awrah (sehemu za siri) ya mtu ni baina ya kitovu na magoti yake. Lakini mtu anapaswa anaposwali avae mavazi mazuri na yaliyo bora kabisa na avae kama wanavyovyaa watu wa nchi aliyoko.”
[Fataawaa Nuwr ‘Alaa Ad-Darb (8/128)]