Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Iyd: Hukmu Ya Wanaume Kukumbatiana Siku Ya 'Iyd, Na Hukmu Ya Kuwabusu Wanawake Walio Maharimu
Iyd: Hukmu Ya Wanaume Kukumbatiana Siku Ya 'Iyd,
Na Hukmu Ya Kuwabusu Wanawake Walio Maharimu
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Ni ipi hukmu ya Wanaume kukumbatiana Siku ya 'Iyd, na kuwabusu Wanawake ambao ni Maharimu?
JIBU:
Na yale wayafanyayo watu Siku ya 'Iyd kwa Wanaume kukumbatiana, hili halina tatizo ndani yake.
Na kuwabusu Wanawake ambao ni Maharimu (ndugu wa damu au wale ambao ni haramu kuwaoa), hakuna ubaya kwa hilo, lakini Wanachuoni wamesema ni karaha (Makruuh) isipokuwa mama, atabusiwa kwenye kichwa chake au kwenye kipaji chake. Na hivyo hivyo (inaruhusiwa) kwa bint na Maharimu wengine.
Iepukwe kuwabusu mashavuni. Hilo ni salama zaidi.
[Majmuw' Fataawa wa Rasaail Ash-Shaykh Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah), Mj.16, uk. 222]