01-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Jinai: Mlango Wa Diya
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلْجِنَايَاتِ
Kitabu Cha Jinai
بَابُ اَلدِّيَاتِ
01-Mlango Wa Diya[1]
1008.
عَنْ أَبِي بَكْرٍ بْنِ مُحَمَّدٍ بْنِ عَمْرِوِ بْنِ حَزْمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ كَتَبَ إِلَى أَهْلِ اَلْيَمَنِ... فَذَكَرَ اَلْحَدِيثَ، وَفِيهِ: {أَنَّ مَنْ اِعْتَبَطَ مُؤْمِنًا قَتْلاً عَنْ بَيِّنَةٍ، فَإِنَّهُ قَوَدٌ، إِلَّا أَنْ يَرْضَى أَوْلِيَاءُ اَلْمَقْتُولِ، وَإِنَّ فِي اَلنَّفْسِ اَلدِّيَةَ مِائَةً مِنْ اَلْإِبِلِ، وَفِي اَلْأَنْفِ إِذَا أُوعِبَ جَدْعُهُ اَلدِّيَةُ، وَفِي اَللِّسَانِ اَلدِّيَةُ، وَفِي اَلشَّفَتَيْنِ اَلدِّيَةُ، وَفِي اَلذِّكْرِ اَلدِّيَةُ، وَفِي اَلْبَيْضَتَيْنِ اَلدِّيَةُ، وَفِي اَلصُّلْبِ اَلدِّيَةُ، وَفِي اَلْعَيْنَيْنِ اَلدِّيَةُ، وَفِي اَلرِّجْلِ اَلْوَاحِدَةِ نِصْفُ اَلدِّيَةِ، وَفِي الْمَأْمُومَةِ ثُلُثُ اَلدِّيَةِ، وَفِي اَلْجَائِفَةِ ثُلُثُ اَلدِّيَةِ، وَفِي اَلْمُنَقِّلَةِ خَمْسَ عَشْرَةَ مِنْ اَلْإِبِلِ، وَفِي كُلِّ إِصْبَعٍ مِنْ أَصَابِعِ اَلْيَدِ وَالرِّجْلِ عَشْرٌ مِنْ اَلْإِبِلِ، وَفِي اَلسِّنِّ خَمْسٌ مِنْ اَلْإِبِلِ وَفِي اَلْمُوضِحَةِ خَمْسٌ مِنْ اَلْإِبِلِ، وَإِنَّ اَلرَّجُلَ يُقْتَلُ بِالْمَرْأَةِ، وَعَلَى أَهْلِ اَلذَّهَبِ أَلْفُ دِينَارٍ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ فِي "اَلْمَرَاسِيلِ" وَالنَّسَائِيُّ، وَابْنُ خُزَيْمَةَ، وَابْنُ اَلْجَارُودِ، وَابْنُ حِبَّانَ، وَأَحْمَدُ، وَاخْتَلَفُوا فِي صِحَّتِهِ
Kutoka kwa Abuu Bakr bin Muhammad bin ‘Amr bin Hazm[2] kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwaandikia watu wa Yemen akaitaja Hadiyth ndani yake inasema: “Kwa hakika mwenye kumuua Muumin bila ushahidi wa kupasa kuuwawa, basi atalipiziwa kisasi, isipokuwa watakaporidhia wasimamizi wa aliyeuwawa.”[3] Katika kuuwa nafsi kuna diya kamili, nayo ni ngamia mia. Katika pua inapokatwa yote kuna diya kamili. Katika macho mawili kuna diya kamili, katika ulimi kuna diya kamili, katika midomo kuna diya kamili. Katika dhakar (uume) kuna diya kamili, katika dhakari ya mwanamume kuna diya kamili, katika uti wa mgongo kuna diya kamili, katika mguu mmoja kuna nusu ya diya. Katika mpasuko uliokaribia ubongo ni thuluthi ya diya. Katika jeraha lililovunja mifupa ni ngamia kumi na tano. Katika kila kidole miongoni mwa vidole vya mikononi na miguuni ni ngamia kumi. Katika jino ni ngamia watano. Katika jeraha linaloonyesha mfupa ni ngamia watano. Na kwa hakika mwanamume anauawa kwa kuuwa mwanamke. Na wenye dhahabu watatoa dinari elfu moja.”[4] [Imetolewa na Abuu Daawuwd katika kitabu cha Al-Maraasiyl, na An-Nasaaiy, Ibn Khuzaymah, Ibn Al-Jaaruwd, Ibn Hibbaan na Ahmad wamekhitilafiana katika kuswihi kwake]
1009.
وَعَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنْ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {دِيَةُ اَلْخَطَأَ أَخْمَاسًا: عِشْرُونَ حِقَّةً، وَعِشْرُونَ جَذَعَةً، وَعِشْرُونَ بَنَاتِ مَخَاضٍ، وَعِشْرُونَ بَنَاتِ لَبُونٍ، وَعِشْرُونَ بَنِي لَبُونٍ} أَخْرَجَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ.
وَأَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ، بِلَفْظٍ: {وَعِشْرُونَ بِنِي مَخَاضٍ} ، بَدَلَ: {بُنِيَ لَبُونٍ} وَإِسْنَادُ اَلْأَوَّلِ أَقْوَى.
وَأَخْرَجَهُ اِبْنُ أَبِي شَيْبَةَ مِنْ وَجْهٍ آخَرَ مَوْقُوفًا، وَهُوَ أَصَحُّ مِنْ اَلْمَرْفُوعِ
وَأَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ: مِنْ طَرِيقِ عَمْرِوِ بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ رَفَعَهُ: {اَلدِّيَةُ ثَلَاثُونَ حِقَّةً، وَثَلَاثُونَ جَذَعَةً، وَأَرْبَعُونَ خَلِفَةً. فِي بُطُونِهَا أَوْلَادُهَا}
Kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Diya ya bahati mbaya ni aina tano: hiqqah[5] ishirini, jadha’ah[6] ishirini, banaati makhaadhw[7] ishirini, banaati labuwni[8] ishirini na baniy labuwni[9] ishirini.” [Imetolewa na Ad Daaraqutwniyy]
Na imepokewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) kwa tamshi: “…na baniy makhaadhw ishirini.” Badala ya: “...bin labuwni.” Isnaad ya Hadiyth ya kwanza ina nguvu.
Na Ibn Abiy Shaybah ameipokea kwa njia nyingine mawquwf ndiyo sahihi zaidi kuliko Marfuw’.
Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy wameipokea kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb naye kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake ikiwa ni Marfuw’: “Ad Diyyah ni hiqqah thalathini na jadha’ah thalathini na ngamia arubaini wenye mimba.”
1010.
وَعَنْ اِبْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، عَنْ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {إِنَّ أَعْتَى اَلنَّاسِ عَلَى اَللَّهِ ثَلَاثَةٌ: مَنْ قَتَلَ فِي حَرَمَ اَللَّهِ، أَوْ قَتَلَ غَيْرَ قَاتِلِهِ، أَوْ قَتَلَ لِذَحْلِ اَلْجَاهِلِيَّةِ} أَخْرَجَهُ اِبْنُ حِبَّانَ فِي حَدِيثٍ صَحَّحَهُ
Kutoka kwa Ibn ‘Amr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika watu wenye majivuno zaidi kwa Allaah ni watatu: mwenye kuuwa katika Haram ya Allaah (Makkah), au akamuuwa asiyeuwa au akauwa kwa kisasi cha kijahiliya.” [Imetolewa na Ibn Hibbaan katika hadiyth aliyoisahihisha]
1011.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {أَلَا إِنَّ دِيَةَ اَلْخَطَأِ شِبْهِ اَلْعَمْدِ مَا كَانَ بِالسَّوْطِ وَالْعَصَا مَائَةٌ مِنَ اَلْإِبِلِ، مِنْهَا أَرْبَعُونَ فِي بُطُونِهَا أَوْلَادُهَا} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Jueni diya ya kuuwa (bahati mbaya)[10] na kuuwa kunakofanana na makusudi inayokuwa kwa mjeledi au fimbo (diya yake ni) ngamia mia, katika hao arubaini wenye mimba.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah, na akaisahihisha Ibn Hibbaan]
1012.
وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، عَنْ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {هَذِهِ وَهَذِهِ سَوَاءٌ يَعْنِي: اَلْخُنْصَرَ وَالْإِبْهَامَ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
وَلِأَبِي دَاوُدَ وَاَلتِّرْمِذِيَّ:{دِيَةُ اَلْأَصَابِعِ سَوَاءٌ، وَالْأَسْنَانُ سَوَاءٌ: اَلثَّنِيَّةُ وَالضِّرْسُ سَوَاءٌ}
وَلِابْنِ حِبَّانَ:{دِيَةُ أَصَابِعِ اَلْيَدَيْنِ وَالرِّجْلَيْنِ سَوَاءٌ، عَشَرَةٌ مِنْ اَلْإِبِلِ لِكُلِّ إصْبَعٍ}
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hiki kwa hiki ni sawa yaani kidole kidogo na kidole gumba.”[11] [Imetolewa na Al Bukhaariy]
Na kutoka kwa Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy: “Diya ya vidole ni sawa, na diya ya meno ni sawa, na diya ya meno ya mbele na magego ni sawa.”
Na Ibn Hibbaan ameipokea: “Diya ya vidole vya mikono na miguu ni sawa na ngamia kumi katika kila kidole.”
1013.
وَعَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ رَفَعَهُ قَالَ: {مَنْ تَطَبَّبَ وَلَمْ يَكُنْ بِالطِّبِّ مَعْرُوفًا فَأَصَابَ نَفْسًا فَمَا دُونَهَا، فَهُوَ ضَامِنٌ} أَخْرَجَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ، وَهُوَ عِنْدَ أَبِي دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيِّ وَغَيْرِهِمَا، إِلَّا أَنَّ مَنْ أَرْسَلَهُ أَقْوَى مِمَّنْ وَصَلَهُ
Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kutibu na si mjuzi wa tiba, akauwa nafsi na kusababisha madhara mengine basi atalipa.”[12] [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniyy na akaisahihisha Al-Haakim. Nayo iko kwa Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy na wengine. Isipokuwa alieifanya kuwa ni Mursal ana nguvu zaidi kuliko aliyeifanya Mawsuwl]
1014.
وَعَنْهُ، أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {فِي الْمَوَاضِحِ خَمْسٌ، خَمْسٌ مِنْ اَلْإِبِلِ} رَوَاهُ أَحْمَدُ. وَالْأَرْبَعَةُ. وَزَادَ أَحْمَدُ:{وَالْأَصَابِعُ سَوَاءٌ، كُلُّهُنَّ عَشْرٌ، عَشْرٌ مِنَ اَلْإِبِلِ} وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ، وَابْنُ اَلْجَارُودِ.
Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Katika majeraha yanayoonesha mfupa ni ngamia watano.” [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah)]
Na akaongezea Ahmad: “Na vidole vyote ni sawa ngamia kumi kumi.” Na akaisahihisha Ibn Khuzaymah na Ibn Al-Jaaruwd.
1015.
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {عَقْلُ أَهْلِ اَلذِّمَّةِ نِصْفُ عَقْلِ اَلْمُسْلِمِينَ} رَوَاهُ أَحْمَدُ وَالْأَرْبَعَةُ
وَلَفْظُ أَبِي دَاوُدَ: {دِيَةُ اَلْمُعَاهِدِ نِصْفُ دِيَةِ اَلْحُرِّ}
وَلِلنِّسَائِيِّ: {عَقْلُ اَلْمَرْأَةِ مِثْلُ عَقْلِ اَلرَّجُلِ، حَتَّى يَبْلُغَ اَلثُّلُثَ مِنْ دِيَتِهَا} وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ
Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Diya ya ahlu adh-dhimmah[13] ni nusu ya diya ya Waislam.” [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah)]
Na katika tamshi la Abuu Daawuwd: “Diya ya aliyewekeana mkataba (Mu’aahid) ni nusu ya diya ya aliye huru.”
Na katika An-Nasaaiy: “Diya ya mwanamke ni sawa na diya ya mwanamume hadi ifikie thuluthi katika diya yake.” Na akaisahihisha Ibn Khuzaymah
1016.
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {عَقْلُ شِبْهِ اَلْعَمْدِ مُغَلَّظٌ مِثْلُ عَقْلِ اَلْعَمْدِ، وَلَا يَقْتَلُ صَاحِبُهُ، وَذَلِكَ أَنْ يَنْزُوَ اَلشَّيْطَانُ، فَتَكُونُ دِمَاءٌ بَيْنَ اَلنَّاسِ فِي غَيْرِ ضَغِينَةٍ، وَلَا حَمْلِ سِلَاحٍ} أَخْرَجَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ وَضَعَّفَهُ
Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Diya ya kuuwa kunakofanana na makusudi ni diya nzito, mfano wa diya ya kuuwa kwa makusudi aliyeuwa hauwawi,[14] ni shari ya shaytwaan, damu ikamwagika baina ya watu bila ya kuwepo chuki wala kubeba silaha.” [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniy na ameidhoofisha]
1017.
عَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {قَتَلَ رَجُلٌ رَجُلًا عَلَى عَهْدِ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فَجَعَلَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ دِيَتَهُ اِثْنَيْ عَشَرَ أَلْفًا} رَوَاهُ اَلْأَرْبَعَةُ، وَرَجَّحَ النَّسَائِيُّ وَأَبُو حَاتِمٍ إِرْسَالَهُ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: Mtu mmoja aliuwa mtu katika zama za Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akahukumu diya yake dirhamu elfu kumi na mbili. [Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah)
1018.
وَعَنْ أَبِي رِمْثَةَ قَالَ: {أَتَيْتُ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ وَمَعِي اِبْنِي فَقَالَ: "مَنْ هَذَا ؟" قُلْتُ: اِبْنِي. أَشْهَدُ بِهِ. قَالَ: "أَمَّا إِنَّهُ لَا يَجْنِي عَلَيْكَ، وَلَا تَجْنِي عَلَيْهِ} رَوَاهُ النَّسَائِيُّ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ، وَابْنُ اَلْجَارُودِ
Kutoka kwa Abuu Rimthah[15] amesema: Nilimuendea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) pamoja na mtoto wangu, akasema: “Huyu ni nani?” Nikasema ni mtoto wangu nami namshuhudia kuwa huyu ni mwanangu. Akasema: “Hutoulizwa kwa kosa lake, naye hatoulizwa kwa kosa lako.”[16] [Imetolewa na An-Nasaaiy na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Ibn Khuzaymah na Ibn Al-Jaaruwd]
[1] Diya ni malipo ya damu iliyomwagwa. Malipo haya yanalipwa kwa warithi wake.
[2] Huyu ni Abuu Bakr bin Muhammad bin ‘Amr bin Hazm Al-Ansari An-Najari Al-Madaniy Al-Qadhwi. Alikuwa madhubuti, mwenye taqwa na alikuwa mmoja katika waliochangia kwa vitabu sita vya Hadiyth. Alikuwa ni taabi’i wa kizazi cha tano. Mke wake anamuelezea kuwa hakuweza kulala kitandani mwake kwa muda wa miaka arubaini, akimaanisha kuwa alikua akiamka visimamo vya usiku. Ibn Ma’in amemtaja kuwa ni madhubuti, na Ibn Sa’ad amesema kuwa alifariki mwaka 120 Hijriyyah.
[3] Katika hii inamaanisha kuwa katika mauaji ya kukusudia, mrithi wa aliyeuwawa bila kujali kama ni wa damu au wa kupanga, wana hiari aina nne: (a) kisasi kwa kuuwawa kwa mkosaji, (b) fidiya, (c) kumsamehe muuwaji, (d) kuwa na utaratibu mwingine wa kulipa zaidi au pungufu ya fidiya.
[4] Hadiyth hii inaelezea misingi ya Shariy’ah na wanaostahiki, kwa mfano mrithi wa aliyeuwawa, aliyeuwawa bila ya kuwepo kwa makosa kwa upande wake, ana uchaguzi ima achukue fidiya au alipe kisasa. Kiwango cha fidiya ni ngamia mia moja au thamani yake. Kuna ibara inayotaja kila jina la kiungo. Al-Ma-muwmah ni pigo linaloathiri akili ya mtu. Al-Jaaifah ni jeraha linalotokana na koo hadi tumboni na kumalizia kienani na kutokozea tumboni. Al-Muwdhwihah ni jeraha linalopasua nyama ya mtu katika mwili na kufanya mfupa uonekane.
[5] Hiqqah ni ngamia jike akiwa katika mwaka wake wa nne
[6] Jadha’ah ni ngamia jike akiwa katika mwaka wake wa tano.
[7] Banaati makhaadhw ni ngamia jike wanaoingia mwaka wao wa pili.
[8] Banaati labuwni ni ngamia jike wanaoingia katika mwaka wao wa tatu.
[9] Baniy labuwni ni ngamia dume anaoingia katika mwaka wake wa tatu.
[10] Hadiyth iliyopokelewa na Ibn Mas-‘uwd kuhusu diya inayolipwa kwa tukio la mauaji kimakosa imetajwa hapo kabla. Baadhi ya watu wakitumia Hadiyth hii wanachukulia fidiya hii kuwa ni sahihi na inaweza kutumika katika hali zote. Mantiki yake ni kuwa kila kesi ya mauaji hushughulikiwa peke yake kulingana na mazingira na hali ya aliyeuliwa. Kwa mfano ikiwa mtu kauwawa katika tukio lisilo la umwagaji damu katika hali iliyokuwa ya amani, basi adhabu yake itakuwa ni kali zaidi. Mauaji ya makusudi ni yale mtu ambayo anadhimiria na kutumia silaha yenye kuuwa na kusababisha mauti kwa mtu. Mauaji ya bahati mbaya ni yale ya mtu kutumia kitu chenye kuuwa lakini hakuwa amekusudia kumuuwa. Kwa mfano mshale, ambao umerushwa kumpiga kiwindwa, ambao ulimkosa na kumpata mwana Aadam. Mauaji ya kukusudia ni yale ya kumkusudia mtu fulani lakin silaha au ala iliyotumika kufanya jambo lile si aghlabu kusababisha kifo kama vile; mjeledi, kirungu na tofali, na kadhalika.
[11] Vidole vyote vina thamani moja katika suala la malipo ya fidiya.
[12] Maadamu si mtaalamu wa tiba, haruhusiwi kufanya kazi yenyewe kwa hatari anayoweza kusababisha. Ikiwa mgonjwa alikuwa anatibiwa na daktari kama huyu akapata matatizo kutokana na operesheni au dawa alizoandikiwa zikamuuwa ni juu ya daktari yule kulipa fidiya.
[13] Hadiyth hii inabainisha mambo mawili. Kwanza, diya kwa Ahl Adh-dhimmah ni nusu anayolipwa Muislam. Dhimmi ni neno linalotumiwa kwa maana ya kafiri anayeishi katika dola ya Kiislam. Pili, fidiya kwa mwanamke aliyejeruhiwa ni sawa na ya mwanamme, hadi itakapofikia kiwango cha theluthi ya fidiya. Chochote kinachozidi theluthi kitaingia katika nusu kama ni fidiya atakayolipwa mtu.
[14] Thamani ya fidiya kwa adhabu hii inategemea hukumu. Katika hali ya matukio ya mauaji yaliyoenea sehemu fulani au ya kwamba mauaji ametokea kuwa ni mtu mwenye tabia mbaya sana ya kikatili, ni juu ya Qadhwi kukadiria fidiya kama ya mauaji ya makusudi. Lakini kama tukio linaonesha kinyume na hivyo, Qadhwi ana uwezo wa kukadiria fidiya ndogo zaidi kama ilivyo katika mauaji yaliyofanyika kwa bahati mbaya na kwa makosa.
[15] Abuu Rimthah: Inasemekana kuwa jina lake ni Habib bin Haiyaan au Rifa’a bin Yathrib au ‘Amaarah bin Yathrib, Balwiy au Taym wa Banu Taym Ar-Rabaab. Inasemekana vile vile kuwa alikuwa Tamimi kizazi cha Amru Al-Qais bin Zayd Manaat bin Tamiym. Alikuwa ni Swahaba aliyekuwa akiishi mji wa Kufa Iraq.
[16] Lengo la kutajwa Hadiyth hii ni kuelezea kuwa mtoto habebi majukumu ya makosa aliyofanya baba yake na vivyo hivyo baba habebi dhambi ya mwanaye. Mtu haadhibiwi kwa makosa ya mwenzake.