02-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Jinai: Mlango Wa Kudai Damu Na Kiapo

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْجِنَايَاتِ

Kitabu Cha  Jinai

 

بَابُ دَعْوَى اَلدَّمِ وَالْقَسَامَةِ

02-Mlango Wa Kudai Damu Na Kiapo

 

 

 

 

 

1019.

عَنْ سَهْلِ بْنِ أَبِي حَثْمَةَ، عَنْ رِجَالٍ مِنْ كُبَرَاءِ قَوْمِهِ، أَنَّ عَبْدَ اَللَّهِ بْنَ سَهْلٍ ومُحَيِّصَةَ بْنَ مَسْعُودٍ خَرَجَا إِلَى خَيْبَرَ مِنْ جَهْدٍ أَصَابَهُمْ، فَأُتِيَ مَحَيِّصَةُ فَأُخْبِرَ أَنَّ عَبْدَ اَللَّهِ بْنِ سَهْلِ قَدْ قُتِلَ، وَطُرِحَ فِي عَيْنٍ، فَأَتَى يَهُودَ، فَقَالَ: أَنْتُمْ وَاَللَّهِ قَتَلْتُمُوهُ.‏ قَالُوا: وَاَللَّهِ مَا قَتَلْنَاهُ، فَأَقْبَلَ هُوَ وَأَخُوهُ حُوَيِّصَةُ وَعَبْدُ اَلرَّحْمَنِ بْنُ سَهْلٍ، فَذَهَبَ مُحَيِّصَةُ لَيَتَكَلَّمَ، فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏{"كَبِّرْ كَبِّرْ" يُرِيدُ: اَلسِّنَّ، فَتَكَلَّمَ حُوَيِّصَةُ، ثُمَّ تَكَلَّمَ مُحَيِّصَةُ، فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏"إِمَّا أَنْ يَدُوا صَاحِبَكُمْ، وَإِمَّا أَنْ يَأْذَنُوا بِحَرْبٍ".‏ فَكَتَبَ إِلَيْهِمْ فِي ذَلِكَ ]كِتَابًا[.‏ فَكَتَبُوا: إِنَّا وَاَللَّهِ مَا قَتَلْنَاهُ، فَقَالَ لِحُوَيِّصَةَ، وَمُحَيِّصَةُ، وَعَبْدِ اَلرَّحْمَنِ بْنَ سَهْلٍ: "أَتَحْلِفُونَ، وَتَسْتَحِقُّونَ دَمَ صَاحِبَكُمْ؟" قَالُوا: لَا.‏ قَالَ: "فَتَحْلِفُ لَكُمْ يَهُودُ؟" قَالُوا: لَيْسُوا مُسْلِمِينَ فَوَدَاهُ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏مِنْ عِنْدِهِ، فَبَعَثَ إِلَيْهِمْ مَائَةَ نَاقَةٍ.‏ قَالَ سَهْلٌ: فَلَقَدْ رَكَضَتْنِي مِنْهَا نَاقَةٌ حَمْرَاءُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ.

Kutoka kwa Sahli bin Abuu Hathmah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kutoka kwa wakubwa wa kabila lake kuwa: ’Abdullaah bin Sahl[1] na Muhayyiswah[2] bin Mas-‘uwd walienda Khaybar kwa sababu ya ukame uliowapata. Muhayyiswah akamuendea ‘Abdullaah bin Sahl akaambiwa kuwa ameuliwa na ametupwa katika kisima. Akawaendea Mayahudi na akawaambia: “Wa-Allaahi nyinyi mumemuuwa.” Mayahudi wakasema: “Wa-Allaahi hatukumuuwa.” Yeye na ndugu yake Huwayyiswah[3] na ‘Abdur-Rahmaan bin Sahl[4] walifika na Muhayyiswah alikuwa anataka kuzungumza na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamkatisha kwa kusema: “Mtangulize mkubwa, mtangulize mkubwa.” Huwayyiswah akazungumza kisha Muhayyisah naye akazungumza. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akawaambia: “Ima waondoe diya ya mwenzenu au watangaziwe vita.” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akawaandikia barua, nao wakajibu: “Wa-Allaahi  sisi hatukumuuwa.” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia Huwayyiswah, Muhayyiswah na ‘Abdur-Rahmaan bin Sahl: “Mtaapa ili mstahiki damu ya mwenzenu?” Wakasema: “Hapana.” Akawaambia: “Basi Mayahudi wataapa.” (kuwa hawakuhusika) wakasema: “Wao sio Waislamu.”  Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) binafsi yake akamlipia diya,[5] akawapelekea ngamia mia. Sahli amesema: “Katika ngamia hao kuna ngamia mwekundu aliyenikanyaga.” [Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

1020.

وَعَنْ رَجُلٍ مِنْ اَلْأَنْصَارِ، {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏أَقَرَّ اَلْقَسَامَةَ عَلَى مَا كَانَتْ عَلَيْهِ فِي اَلْجَاهِلِيَّةِ، وَقَضَى بِهَا رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏بَيْنَ نَاسٍ مِنَ اَلْأَنْصَارِ فِي قَتِيلٍ اِدَّعَوْهُ عَلَى اَلْيَهُودِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa mtu mmoja katika Answaar amesema kuwa: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekiri Qasaamah iliyokuwa katika zama za ujahiliya[6] na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amehukumu kwa hiyo Qasaamah (kiapo katika kesi za mauaji) baina ya watu mongoni mwa Answaar kuhusu mtu wao aliyeuwawa waliodai kuwa waliomuuwa ni mayahudi. [Imetolewa na Muslim]

 

[1] ’Abdullaah bin Sahl bin Zaid bin Ka’ab bin ‘Aamir Al-Answaar Al-Haarith aliuwawa Khaybar na mwili wake ulipatikana katika chemchem huku shingo yake ikionekana imevunjwa.

[2] Abu Sa’iyd Muhayyiswah bin Mas-‘uwd bin Ka’ab Al-Haarith Al-Answaar Al-Madaniy, ni jamaa wa Swahaba aliyeuwawa; ‘Abdullaah ambaye alisilimu kabla ya Hijra na alishiriki katika vita vya Uhud, Al-Khandaq na vita vingine muhimu vilivyobakia. Rasuli wa Allaah alimtuma Fadak kuenda kuwalingania watu katika Uislamu.

[3] Huyu alikuwa ni kaka wa Muhayyiswah alisilimu kwa msaada wa ndugu yake. Inasemekana alishiriki katika vita vya Khandaq, Uhud na vita vingine muhimu pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).

[4] Huyu ni kaka yake ‘Abdullaah bin Sahl mama yake akiitwa Laylah, binti wa Nafi bin ‘Aamir. Inasemekana kuwa alipigana katika vita vya Badr, Uhud na vita vingine vyote muhimu. Aliumwa na nyoka na ‘Amaara bin Hazm alimtibu kwa Ruqyah kwa maelekezo kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Hata hivyo, Ibn Hajar aliingiwa na wasiwasi wa kuipokea na kuweka katika kitabu chake Al-Iswaabah.

[5] Qasaamah ina maana ya masharti ambapo muuaji hajafahamika, mtuhumiwa au watu husika au watu wa kabila fulani  wanatakiwa watoe kiapo. Tukio kama hili linapotokea, watu hamsini wanatakiwa wajitokeze ili waape ya kwamba wao au watu wa kijiji hawajafanya mauaji hayo. Aina hii ya viapo vinatumika mahakamani tu. Viapo hivi havitumiki katika aina zingine za adhabu (huduwd). Qasaamah inatekelezwa na watu wawili (mlalamikaji au mlalamikiwa). Ikiwa mlalamikaji (warithi wa marehemu) watatoa ushahidi, au watatumia kiapo kama ushahidi haupo kuwa hawa ndio wauaji wenyewe, bila shaka itakuwa wazi kwa wanaojitetea kuwa ni wajibu kwao kulipa fidiya kwa walalamikaji. Walalamikaji wakishindwa kufanya hivyo, walalamikiwa wanatakiwa kuleta watu wapatao hamsini kisha waape kuwa hawajaua. Kiapo kilichotajwa kitatolewa na wale watu waliochaguliwa na muombaji mwenyewe. Hii ndio hukumu pekee inayohalalisha kiapo kwa upande wa muombaji vile vile.

[6] Katika hali hii, Shariy’ah inakubali kiapo kitakachoapwa na kafiri. Qasaamah haifanyi kazi kwa tuhuma zitakazoletwa na muombaji ila itakapokuwa imeambatanishwa na ushahidi mzito unaohusiana na mauaji.

Share