03-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Jinai: Mlango Wa Kuwapiga Vita Waasi (Wa Kiongozi)
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلْجِنَايَاتِ
Kitabu Cha Jinai
بَابُ قِتَالِ أَهْلِ اَلْبَغْيِ
03-Mlango Wa Kuwapiga Vita Waasi (Wa Kiongozi)
1021.
عَنْ اِبْنِ عُمَرَ رِضَيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {مَنْ حَمَلَ عَلَيْنَا اَلسِّلَاحَ، فَلَيْسَ مِنَّا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kutubebea silaha si katika sisi.”[1] [Bukaariy, Muslim]
1022.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنْ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {مَنْ خَرَجَ عَنْ اَلطَّاعَةِ، وَفَارَقَ اَلْجَمَاعَةَ، وَمَاتَ، فَمِيتَتُهُ مِيتَةٌ جَاهِلِيَّةٌ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kutoka katika utiifu (wa kiongozi) na akajitenga na jamaa na akafariki, basi kifo chake ni kifo cha kijahiliya.”[2] [Imetolewa na Muslim]
1023.
وَعَنْ أَمِّ سَلَمَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {تَقْتُلُ عَمَّارًا اَلْفِئَةُ اَلْبَاغِيَةُ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Ummu Salamah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “’Ammaar atauwawa na kikundi kilichoasi (kiovu).”[3] [Imetolewa na Muslim]
1024.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {هَلْ تَدْرِي يَا اِبْنَ أُمِّ عَبْدٍ، كَيْفَ حُكْمُ اَللَّهِ فِيمَنْ بَغَى مِنْ هَذِهِ اَلْأُمَّةِ ؟ "، قَالَ: اَللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ. قَالَ: "لَا يُجْهَزُ عَلَى جَرِيحِهَا، وَلَا يُقْتَلُ أَسِيرُهَا، وَلَا يُطْلَبُ هَارِبُهَا، وَلَا يُقْسَمُ فَيْؤُهَا} رَوَاهُ اَلْبَزَّارُ و اَلْحَاكِمُ وَصَحَّحَهُ فَوَهِمَ، فَإِنَّ فِي إِسْنَادِهِ كَوْثَرَ بْنَ حَكِيمٍ، وَهُوَ مَتْرُوكٌ وَصَحَّ عَنْ عَلِيٍّ مِنْ طُرُقٍ نَحْوُهُ مَوْقُوفًا. أَخْرَجَهُ اِبْنُ أَبِي شَيْبَةَ، وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ee mwana wa Ummi ‘Abd (‘Abdullaah bin Mas-‘uwd), unajua nini hukumu ya Allaah kwa aliyeasi katika ummah huu? Akasema Allaah na Rasuli wa Allaah Wanajua. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Aliyejeruhiwa hamalizwi, mateka wake hauliwi, aliyekimbia hafuatwi na mali yake haigawanywi.”[4] [Imetolewa na Al-Bazzaar na Al-Haakim na akaisahihisha akaghafilika kwa sababu katika isnaad yake yumo Kawthar[5] bin Hakiym ambaye Hadiyth zake zinaachwa. Lakini imeswihi kutoka kwa ‘Aliy kwa njia nyingine mfano wa Hadiyth kama hii ikiwa ni Mawquwf iliyopokewa na Ibn Abiy Shaybah na Al-Haakim]
1025.
وَعَنْ عَرْفَجَةَ بْنِ شُرَيْحٍ: سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ يَقُولُ: {مَنْ أَتَاكُمْ وَأَمَرَكُمْ جَمِيعٌ، يُرِيدُ أَنْ يُفَرِّقَ جَمَاعَتَكُمْ، فَاقْتُلُوهُ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa ‘Arfajah bin Shurayh[6] amesema kuwa alimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Atakayewajia nyinyi na jambo lenu ni moja, na anataka kuwatenganisha katika umoja wenu, basi mpigeni vita.” [Imetolewa na Muslim]
[1] Kupigana dhidi ya Shariy’ah ni dhambi kubwa. Vivyo hivyo, kumtishia Muislam kumuuwa au kumtolea silaha ni dhambi kubwa. Ikiwa mtu amehalalisha damu ya Muislam au kumuuwa kwa kuona kuwa ni halaal kufanya hivyo, bila shaka mtu huyu atakuwa ameritadi. Mtu huyu anazingatiwa kuwa amekufuru kwa makubaliano ya Jamhuri ya ‘Uamaa. Hata hivyo ni halaal kuwapiga Waislam walioasi dhidi ya mamlaka ya Shariy’ah kama ilivyokuja katika Qur-aan:
فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّىٰ تَفِيءَ إِلَىٰ أَمْرِ اللَّـهِ ۚ
“…basi piganeni na ambalo linakandamiza mpaka lielemee kwenye amri ya Allaah…” [Al-Hujuraat: 9]. Kadhalika tunajifunza hayo katika Hadiyth mbalimbali.
[2] Utiifu kwa Amiri (mtawala) ni wajibu madamu hajakwenda kinyume na Shariy’ah za Kiislam. Vivyo hivyo, hairuhusiwi kutoka katika jamaa, maadamu hafanyi yanayoweza kumtoa katika Uislam. Kwa kumkaidi Amiri anayetawala kwa misingi ya Shariy’ah ya Kiislam ni uasi. Yeyote anayevunja mamlaka ya Amiri au kujitoa katika kundi pamoja na kuwa hatoonekana kuwa ni kafiri lakini ataonekana kuwa amekwenda kombo. Tofauti yao ni kuwa si katika wao mwenye Imaam au mamlaka ya kishariy’ah.
[3] Aliuwawa katika vita vya Swiffiyn na wale waliokuwa wakipigana dhidi ya ‘Aliy.
[4] Hakuna kutokubaliana kuhusu uhalali wa kuwapiga vita watu waliodhulumu. Hata hivyo, kuna tofauti ya maoni kwa ‘Ulamaa katika kumata mali zao, kuwaacha waliojeruhiwa na kuwashawishi wanaotaka kutoroka.
[5] Alikuwa ni mkazi wa mji wa Kufa uliopo ‘Iraq na baadae akahamia Halab. Ibn Ma’iyn anamzungumzia, “Si chochote katika Hadiyth.” Ahmad bin Hanbal naye anamsema: “Hadiyth zake ni za uongo.”
[6] ‘Arfajah bin Shurayh Ashja’i alikuwa ni Swahaba aliyekuwa akiishi Kufa (mji uliopo Iraq).