04-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Jinai: Mlango Wa Kupigana Na Anayefanya Jinai Na Kumuuwa Aliyeritadi

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْجِنَايَاتِ

Kitabu Cha  Jinai

 

بَابُ قِتَالِ اَلْجَانِي وَقَتْلُ اَلْمُرْتَدِّ

04-Mlango Wa Kupigana Na Anayefanya Jinai Na Kumuuwa Aliyeritadi

 

 

 

 

 

1026.

عَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏{مِنْ قُتِلَ دُونَ مَالِهِ فَهُوَ شَهِيدٌ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anayeuliwa kwa kutetea mali yake, huyo ni Shahiyd.”[1] [Imetolewa na Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na At-Tirmidhiy na akaisahihisha At-Tirmidhiy]

 

 

 

1027.

وَعَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {قَاتَلَ يُعْلَى بْنُ أُمِّيَّةَ رَجُلًا، فَعَضَّ أَحَدُهُمَا صَاحِبَهُ، فَنَزَعَ ثَنِيَّتَهُ، فَاخْتَصَمَا إِلَى اَلنَّبِيِّ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏فَقَالَ: "أَيَعَضُّ أَحَدُكُمْ أَخَاهُ كَمَا يَعَضُّ اَلْفَحْلُ ؟ لَا دِيَةَ لَهُ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ

Kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: Yu’laa bin Ummiyyah alipigana na mtu, mmoja wao akang’ata mkono wa mwingine, akauvuta mkono wake kutoka mdomoni mwake, meno yake ya mbele yakadondoka. Wakashtakiana kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Mmoja wenu anang’ata kama fahali ang’atavyo, mtu huyo hana diya.”[2] [Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

 

 

1028.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ ‏ قَالَ: قَالَ أَبُو اَلْقَاسِمِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏{لَوْ أَنَّ اِمْرَأً اِطَّلَعَ عَلَيْكَ بِغَيْرِ إِذْنٍ، فَحَذَفْتَهُ بِحَصَاةٍ، فَفَقَأْتَ عَيْنَهُ، لَمْ يَكُنْ عَلَيْكَ جُنَاحٌ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ .‏

 وَفِي لَفْظٍ لِأَحْمَدَ، وَالنَّسَائِيِّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ: {فَلَا دِيَةَ لَهُ وَلَا قِصَاصَ}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Lau mtu atakuchungulia bila ruhusa na ukamrushia kijiwe ukaliharibu jicho lake, basi huna dhambi.”[3] [Bukhaariy, Muslim]

Na katika tamshi la Ahmad na An-Nasaaiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan imesema: “Hana diya wala kulipiza kisasi.”

 

 

 

1029.

وَعَنْ اَلْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {قَضَى رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏أَنَّ حِفْظَ اَلْحَوَائِطِ بِالنَّهَارِ عَلَى أَهْلِهَا، وَأَنْ حِفْظَ اَلْمَاشِيَةِ بِاللَّيْلِ عَلَى أَهْلِهَا، وَأَنَّ عَلَى أَهْلِ اَلْمَاشِيَةِ مَا أَصَابَتْ مَاشِيَتُهُمْ بِاللَّيْلِ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ إِلَّا اَلتِّرْمِذِيُّ،‏  وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ وَفِي إِسْنَادِهِ اِخْتِلَافٌ

Kutoka kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alihukumu kuwa kuhifadhi mashamba wakati wa mchana ni jukumu la wenyewe, na kuhifadhi wanyama wakati wa usiku ni jukumu la wenyewe, na kwamba wenye wanyama watalipa kilichoharibiwa na wanyama wao iwapo wameharibu wakati wa usiku.[4] [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa At-Tirmidhiy, na akaisahihisha Ibn Hibbaan na katika isnaad yake kuna tofauti]

 

 

 

1030.

وَعَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ ‏ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ ‏ ‏فِي رَجُلٍ أَسْلَمَ ثُمَّ تَهَوَّدَ‏: {لَا أَجْلِسُ حَتَّى يُقْتَلَ، قَضَاءُ اَللَّهِ وَرَسُولِهِ، فَأُمِرَ بِهِ، فَقُتِلَ}‏ مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَفِي رِوَايَةٍ لِأَبِي دَاوُدَ: {وَكَانَ قَدْ اُسْتُتِيبَ قَبْلَ ذَلِكَ}

Kutoka kwa Mu’aadh bin Jabl (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuhusu mtu aliyesilimu kisha akawa myahudi: “Sitakaa hadi auwawe,[5] hiyo ndiyo hukumu ya Allaah na Rasuli wa Allaah.” Baada ya hapo ikaamriwa auwawe. [Al-Bukhaariy, Muslim]

Na katika riwaayah ya Abuu Daawuwd inasema: “Kabla ya kuuwawa alipewa nafasi ya kutubia.”

 

 

 

1031.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏{مَنْ بَدَّلَ دِينَهُ فَاقْتُلُوهُ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuritadi (kuacha Uislam- anaingia katika Uislam kwa hadaa kwa lengo la kurudi katika dini yake na kuanza kuukejeli na kuutukana Uislam) muuweni.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

1032.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ، {أَنَّ أَعْمَى كَانَتْ لَهُ أُمُّ وَلَدَ تَشْتُمُ اَلنَّبِيَّ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏وَتَقَعُ فِيهِ، فَيَنْهَاهَا، فَلَا تَنْتَهِي، فَلَمَّا كَانَ ذَاتَ لَيْلَةٍ أَخْذَ اَلْمِعْوَلَ، فَجَعَلَهُ فِي بَطْنِهَا، وَاتَّكَأَ عَلَيْهَا فَقَتَلَهَا فَبَلَغَ ذَلِكَ اَلنَّبِيَّ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏فَقَالَ:"أَلَّا اِشْهَدُوا أَنَّ دَمَهَا هَدَرٌ}‏ رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ وَرُوَاتُهُ ثِقَاتٌ.

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Kulikuwa kuna kipofu aliyekuwa na mjakazi, mjakazi huyu alikuwa akimtukana Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na akimdhalilisha. Alikuwa akimkataza bila kukatazika. Usiku mmoja alichukua mtaimbo akauweka juu ya tumbo lake (mjakazi) akaliegemea juu yake akamuuwa. Hili likamfikia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Fahamuni! Shuhudieni kwa hakika damu yake (mjakazi huyo) ni halaal.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd wapokezi wake ni madhubuti]

 

[1] Katika Hadiyth nyingine yenye mnasaba kama huu inasema: “Atakayeuwawa kwa ajili ya mali yake, nafsi, familia na dini yake huyo ni shahidi, na hivyo anastahiki Jannah.” Ikiwa jambazi atamshambulia mtu na kutaka kuchukua mali yake, mke au watoto wake, na mtu yule akajilinda na kumuuwa yule adui katika hali ile hatokuwa ni mwenye dhambi. Hukumu hii ni makubaliano ya Jamhuri ya ‘Ulamaa.   

[2] Ikiwa mtu atajilinda na jambo fulani kisha mwenzake akapata madhara kwa ajili hiyo huwa hakuna fidiya.

[3] Hii inahusu sehemu ambazo huwezi kuingia bila ya ruhusa kama vile nyumba ya mtu au sehemu ya mtu maalum.

[4] Hadiyth hii inamaanisha kuwa ikiwa kundi la wanyama litaharibu mazao au shamba la mtu wakati wa mchana, basi mwenye wanyama hatolipa chochote. Hii ni kwa sababu kwa ada ya wanyama ni kupata malisho yao wakati wa mchana. Katika hali hii mwenye shamba ndiye anayetakiwa kuwa makini na shamba lake zaidi. Vivyo hivyo ni muhimu mtu kulinda wanyama wake usiku kwani kwa wakati huo wanyama wakisababisha madhara ni wajibu wake kulipa.

[5] Hadiyth hii na inayofuatia imepokewa na Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) ambazo zinaeleza kwa uwazi kabisa kuwa adhabu ya aliyeritadi ni kuuliwa. Ikiwa mtu kalazimishwa kuwa hivyo au kusema maneno ya kuonyesha kuwa ameritadi, mtu huyo atasamehewa na Shariy’ah. Baadhi ya ‘Ulamaa wanaona kuwa mwanamke aliyeritadi haadhibiwi. Muono huu sio sahihi kwani naye anaadhibiwa kwa makubaliano ya ‘Ulamaa.

Share