02-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Al-Huduwd (Adhabu): Mlango Wa Adhabu Ya Kusingizia
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلْحُدُودِ
Kitabu Cha Al-Huduwd (Adhabu)
بَابُ حَدِّ اَلْقَذْفِ
02-Mlango Wa Adhabu Ya Kusingizia
1048.
عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {لَمَّا نَزَلَ عُذْرِي، قَامَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ عَلَى اَلْمِنْبَرِ، فَذَكَرَ ذَلِكَ وَتَلَا اَلْقُرْآنَ، فَلَمَّا نَزَلَ أَمَرَ بِرَجُلَيْنِ وَاِمْرَأَةٍ فَضُرِبُوا اَلْحَدَّ} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ وَالْأَرْبَعَةُ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: Udhuru wangu ulipoteremka (kutoka mbinguni)[1] Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisimama juu ya mimbari akaeleza hilo akasoma Qur-aan, alipoteremka aliamuru wanaume wawili na mwanamke mmoja[2] wapigwe haddi (adhabu).[3] [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah)]
1049.
وَعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {أَوَّلَ لِعَانٍ كَانَ فِي اَلْإِسْلَامِ أَنَّ شَرِيكَ بْنُ سَمْحَاءَ قَذَفَهُ هِلَالُ بْنُ أُمَيَّةَ بِاِمْرَأَتِهِ، فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ "اَلْبَيِّنَةَ وَإِلَّا فَحَدٌّ فِي ظَهْرِكَ "} اَلْحَدِيثَ أَخْرَجَهُ أَبُو يَعْلَي، وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ
وَهُوَ فِي اَلْبُخَارِيِّ نَحْوُهُ مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ عَبَّاسٍ
Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Kulaaniana kwa kwanza katika Uislam ni Hilaal bin Umayyah[4] alipomsingizia mke wake kuzini na Shariyka bin Samhaa,[5] Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia: “Leta ushahidi vinginevyo utapigwa mijeledi mgongoni mwako…”[6] mpaka mwisho wa Hadiyth [Imetolewa na Abuu Ya’laa na wapokezi wake ni madhubuti, na katika Al-Bukhaariy kuna Hadiyth kama hii kutoka kwa Ibn ‘Abbaas]
1050.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَامِرٍ بْنِ رَبِيعَةَ قَالَ: {لَقَدْ أَدْرَكَتُ أَبَا بَكْرٍ، وَعُمَرَ، وَعُثْمَانَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمْ، وَمِنْ بَعْدَهُمْ، فَلَمْ أَرَهُمْ يَضْرِبُونَ اَلْمَمْلُوكَ فِي اَلْقَذْفِ إِلَّا أَرْبَعِينَ} رَوَاهُ مَالِكٌ، وَالثَّوْرِيُّ فِي "جَامِعِهِ"
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Aamir bin Rabiy’ah amesema: Nilimkuta Abuu Bakr, ‘Umar na ‘Uthmaan (رضيَ اللهُ عَنْهُمْ) na waliokuja baada yao sikuwaona wakimpiga mtumwa katika adhabu ya kusingizia uzinifu isipokuwa mijeledi arubaini tu.[7] [Imetolewa na Maalik na Ath-Thawriy katika kitabu chake cha Al-Jaami’i]
1051.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {مِنْ قَذْفَ مَمْلُوكَهُ يُقَامُ عَلَيْهِ اَلْحَدُّ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ، إِلَّا أَنْ يَكُونَ كَمَا قَالَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Atakaemsingizia (uzinifu) mtumwa wake atasimamishiwa haddi Siku Ya Qiyaamah[8] isipokuwa iwe ni kama alivyosema.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
[1] Soma Suwrah An-Nuwr Aayah ya 11 (na zinazofuatia)
إِنَّ الَّذِينَ جَاءُوا بِالْإِفْكِ عُصْبَةٌ مِّنكُمْ ۚ لَا تَحْسَبُوهُ شَرًّا لَّكُم ۖ بَلْ هُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُم مَّا اكْتَسَبَ مِنَ الْإِثْمِ ۚ وَالَّذِي تَوَلَّىٰ كِبْرَهُ مِنْهُمْ لَهُ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١١﴾
“Hakika wale walioleta singizo la kashfa; (kumzulia mama wa waumini ‘Aaishah رضي الله عنها) ni kundi miongoni mwenu. Msiichukulie kuwa ni shari kwenu, bali ni khayr kwenu. Kila mtu katika wao atapata yale aliyochuma katika dhambi. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao atapata adhabu kuu.”
[2] Mwanamme anayetajwa hapa ni Mistwah bin Uthaathah na Hassan bin Thaabit na mwanamke aliyekuwa akiitwa Hamna bin Jahsh.
[3] Ikiwa mtu kamtuhumu mtu kwa uzinifu na akashindwa kuthibitisha, itabidi alete mashahidi wane, adhabu yake itakuwa mijeledi themanini. Baadhi ya wanafiki walimsingizia Mama ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) kwa uzinifu. Walitangaza na jambo hilo likawaathiri watu wengi na minong’ono ikawa mingi kuhusu jambo hilo. Pindi ‘Aaishah alipokoshwa na Aayah za Allaah, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitangaza adhabu kali kwa Waumini lakini hakusema chochote kuhusu wanafiki, kwani aliacha adhabu yao wapewe na Allaah. Waumini watatu walioadhibiwa kwa kusingizia huku walikuwa ni Hassan bin Thaabit, Mistwah bin Uthaathah na Hamna bint Jahsh (Radhwiya-Allaahu ‘anhum).
[4] Alikuwa katika Al-Answaar, Aws na Waqifi alikuwa Swahaba mashuhuri. Alisilimu mapema na alikuwa na tabia ya kuyavunja masanamu ya Baniy Waqifu. Alishuhudia vita vya Badr, Uhud na alibeba bendera ya Banu Waqifu katika siku ya Fat-hu Makkah. Alikuwa mmoja kati ya watatu walioshindwa kuhudhuria vita vya Tabuwk ambae altengwa kwa muda wa siku hamsini na baadae walisamehewa na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)
[5] Alikuwa katika kabila la Balawi waliokuwa na ushirika na Answaar. Hilaal bin Umayyah alimtuhumu kuzini na mke wake. Inasemekana kuwa alishiriki katika vita va Uhud na baba yake. Alikuwa na udugu upande wa mama ni pamoja na Baraa bin Maalik, jina la baba yake ni ‘Abaadah bin Mu’tib na As-Sahma lilikuwa ni jina la mama yake.
[6] Ikiwa mtu atamtuhumu mke wake kuzini ni lazima athibitishe kwa ushahidi, vinginevyo au apate laana ya Allaah kwake kwa kumsingizia mke wake. Vinginevyo ataadhibiwa kwa kusingizia. Akimtaja mtu kama ndio mshirika wake katika jinai ile, anatakiwa atoe ushahidi hadi mwisho wake. Kwa kuwa ni mke wake anaweza kukwepa adhabu ya mijeledi lakini hatokwepa laana ya Allaah kwake (ikiwa atakuwa amemsingizia). Nini hali ya mtu aliyetuhumiwa kuwa mshirika wa jinai hii? Hana uchaguzi isipokuwa: (a) Atoe ushahidi kuunga madai yake, au (b) awe tayari kukabiliana na adhabu ya kusingizia.
[7] Hii inathibitisha kuwa adhabu anayopewa mtumwa mwanamme au mwanamke ni nusu ya adhabu apewayo mtu aliyekuwa huru, na hii ni kwa mujibu wa Jamhuri ya ‘Ulamaa.
[8] Hii ina maana kama mtu atamsingizia mtumwa au kijakazi wake kwa uzinifu hatoadhibiwa hapa duniani.