03-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Al-Huduwd (Adhabu): Mlango Wa Adhabu Ya Kuiba
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلْحُدُودِ
Kitabu Cha Al-Huduwd (Adhabu)
بَابُ حَدِّ اَلسَّرِقَةِ
03-Mlango Wa Adhabu Ya Kuiba
1052.
عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ : {لَا تُقْطَعُ يَدُ سَارِقٍ إِلَّا فِي رُبُعِ دِينَارٍ فَصَاعِدًا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ. وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ . وَلَفْظُ اَلْبُخَارِيِّ: "تُقْطَعُ اَلْيَدُ فِي رُبُعِ دِينَارٍ فَصَاعِدًا "
وَفِي رِوَايَةٍ لِأَحْمَدَ "اِقْطَعُوا فِي رُبُعِ دِينَارٍ، وَلَا تَقْطَعُوا فِيمَا هُوَ أَدْنَى مِنْ ذَلِكَ"
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mkono wa mwizi haukatwi ila kwa robo dinari na zaidi.”[1] [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]
Na Matini ya Bukhaariy inasema: “Mkono wa mwizi unakatwa kwa robo dinari na zaidi.”
Na katika riwaayah nyingine ya Ahmad: “Kateni (mkono) katika robo dinari wala msikate chini ya hiyo.”
1053.
وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا: {أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَطَعَ فِي مِجَنٍ، ثَمَنُهُ ثَلَاثَةُ دَرَاهِمَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikata (mkono) katika (kuiba) ngao thamani yake ni dirhamu tatu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
1054.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَعَنَ اَللَّهُ السَّارِقَ ؛ يَسْرِقُ الْبَيْضَةَ ، فَتُقْطَعُ يَدُهُ ، وَيَسْرِقُ الْحَبْلَ ، فَتُقْطَعُ يَدُهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ أَيْضًا
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah Amlaani mwizi! Anaiba yai mkono wake ukakatwa, na anaiba kamba mkono wake ukakatwa.”[2] [Al-Bukhaariy, Muslim]
1055.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا ؛ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {أَتَشْفَعُ فِي حَدٍ مِنْ حُدُودِ الْلَّهِ ؟ " ثُمَّ قَامَ فَاخْتَطَبَ ، فَقَالَ : " أَيُّهَا النَّاسُ ! إِنَّمَا هَلَكَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ أَنَّهُمْ كَانُوا إِذَا سَرَقَ فِيهِمُ الشَّرِيفُ تَرَكُوهُ ، وَإِذَا سَرَقَ فِيهِمُ الضَّعِيفُ أَقَامُوا عَلَيْهِ الْحَدَّ . . .} الْحَدِيثَ . مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ وَلَهُ مِنْ وَجْهٍ آخَرَ : عَنْ عَائِشَةَ : كَانَتِ امْرَأَةٌ تَسْتَعِيرُ الْمَتَاعَ ، وَتَجْحَدُهُ ، فَأَمَرَ الْنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ بِقَطْعِ يَدِهَا
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema (kwa Usaamah Bin Zayd): “Unaombea[3] katika haddi (adhabu) miongoni mwa haddi za Allaah? Halafu akasimama kuwakhutubia watu: ‘Enyi watu! Kwa yakini waliangamia waliokuwa kabla yenu, kwani anapoiba mtukufu wao wanamuacha, na akiiba mnyonge wanamsimamishia haddi.”[4] [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]
Naye Muslim amepokea kwa njia nyingine kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا): “Mwanamke alikuwa akiazima vyombo na anakanusha, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaamuru akatwe mkono.”
1056.
وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {لَيْسَ عَلَى خَائِنٍ وَلَا مُنْتَهِبٍ ، وِلَا مُخْتَلِسٍ ، قَطْعٌ} رَوَاهُ أَحْمَدُ ، وَالْأَرْبَعَةُ ، وَصَحَّحَهُ التِّرْمِذِيُّ ، وَابْنُ حِبَّانَ
Kutoka kwa Jabair (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kufanya khiyana, mwenye kudokoa na mwenye kunyang’anya, hawakatwi mkono.”[5] [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na akaisahihisha At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan]
1057.
وَعَنْ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ ، قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ يَقُولُ: {لَا قَطْعَ فِي ثَمَرٍ وَلَا كَثَرٍ} رَوَاهُ اَلْمَذْكُورُونَ، وَصَحَّحَهُ أَيْضًا اَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ حِبَّانَ
Kutoka kwa Raafi’ bin Khadiyj (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Hakuna kukata mkono kwa aliyechukua matunda wala joyo la mtende.”[6] [Imetolewa na hao waliotajwa, vile vile At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan wameisahihisha]
1058.
وَعَنْ أَبِي أُمَيَّةَ الْمَخْزُومِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {أُتِيَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ بِلِصٍّ قَدِ اعْتَرَفَ اعْتِرَافًا، وَلَمْ يُوجَدْ مَعَهُ مَتَاعٌ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ "مَا إِخَالَكَ سَرَقْتَ". قَالَ: بَلَى، فَأَعَادَ عَلَيْهِ مَرَّتَيْنِ أَوْ ثَلَاثًا، فَأَمَرَ بِهِ فَقُطِعَ. وَجِيءَ بِهِ، فَقَالَ: "اسْتَغْفِرِ اللَّهَ وَتُبْ إِلَيْهِ"، فَقَالَ: أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ، فَقَالَ: "اللَّهُمَّ تُبْ عَلَيْهِ" ثَلَاثًا} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ وَاللَّفْظُ لَهُ، وَأَحْمَدُ، وَالنَّسَائِيُّ، وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ
وَأَخْرَجَهُ الْحَاكِمُ مِنْ حَدِيثِ أَبِي هُرَيْرَةَ، فَسَاقَهُ بِمَعْنَاهُ، وَقَالَ فِيهِ: {اذْهَبُوا بِهِ، فَاقْطَعُوهُ، ثُمَّ احْسِمُوهُ}. وَأَخْرَجَهُ الْبَزَّارُ أَيْضًا، وَقَالَ: لَا بَأْسَ بِإِسْنَادِهِ
Kutoka kwa Abiy Umayyah Al-Makhzuwmiy[7] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliletewa mwizi aliyeungama kuwa aliiba lakini hakuwa na alichoiba, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia: ‘Sidhani kama umeiba’ yule mtu akasema: ‘Nimeiba,[8] akarudia kusema hivyo mara mbili au mara tatu. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaamrisha akatwe mkono kisha akaletwa, akamuambia: ‘Omba msamaha kwa Allaah na utubie Kwake’ yule mtu akasema: ‘Naomba msamaha kwa Allaah na natubia Kwake’ Rasuli wa Allaah akasema: ‘Ee Allaah! Mkubalie tawbah yake’ alisema hivyo mara tatu.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, na matini ya hadiyth ni yake, vile vile imepokewa na Ahmad na An-Nasaaiy na wapokezi wake ni madhubuti]
Pia Al-Haakim ameipokea kutoka katika hadiyth ya Abuu Hurayrah akayieleza ki maana, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akawaambia: “Mchukueni mumkate kisha mumpisheni.” Vile vile Al-Bazzaar ameipokea na amesema: Isnaad yake haina ubaya.
1059.
وَعَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَوْفٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ؛ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {لَا يَغْرَمُ السَّارِقُ إِذَا أُقِيمَ عَلَيْهِ الْحَدُّ} رَوَاهُ النَّسَائِيُّ، وَبَيَّنَ أَنَّهُ مُنْقَطِعٌ. وَقَالَ أَبُو حَاتِمٍ: هُوَ مُنْكَرٌ
Kutoka kwa ‘Abd Ar-Rahmaan bin ‘Awf (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwizi harudishi alichokiiba atakaposimamishiwa[9] haddi.” [Imetolewa na An-Nasaaiy na ameeleza kuwa Hadiyth hii ni Munqatwi’. Na amesema Abuu Haatim: “Hadiyth hii ni Munkar.”]
1060.
وَعَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ؛ {أَنَّهُ سُئِلَ عَنِ التَّمْرِ الْمُعَلَّقِ؟ فَقَالَ: "مَنْ أَصَابَ بِفِيهِ مِنْ ذِي حَاجَةٍ، غَيْرَ مُتَّخِذٍ خُبْنَةً، فَلَا شَيْءَ عَلَيْهِ، وَمَنْ خَرَجَ بِشَيْءٍ مِنْهُ، فَعَلَيْهِ الْغَرَامَةُ وَالْعُقُوبَةُ، وَمَنْ خَرَجَ بِشَيْءٍ مِنْهُ بَعْدَ أَنْ يُؤْوِيَهُ الْجَرِينُ، فَبَلَغَ ثَمَنَ الْمِجَنِّ فَعَلَيْهِ الْقَطْعُ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ الْحَاكِمُ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliulizwa kuhusu tende zilizotundikwa, akasema: “Mwenye haja akila kiasi cha haja bila ya kuchukua hana lawama. Na mwenye kutoka na kitu basi atapata kulipa na kuadhibiwa. Na mwenye kuchukua sehemu (katika hiyo tende) baada ya kuingizwa sehemu inayokaushiwa na ikafikia thamani ya tende zinazotiwa sehemu hiyo, basi atakatwa (mkono).” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy na akaisahihisha Al-Haakim]
1061.
وَعَنْ صَفْوَانَ بْنِ أُمِّيَّةٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ لَهُ لَمَّا أَمَرَ بِقَطْعِ اَلَّذِي سَرَقَ رِدَاءَهُ، فَشَفَعَ فِيهِ: {هَلَّا كَانَ ذَلِكَ قَبْلِ أَنْ تَأْتِيَنِي بِهِ} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةَ. وَصَحَّحَهُ اِبْنُ اَلْجَارُودِ، وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa Swafwaan bin Ummiyyah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipoamrisha kukatwa mkono wa aliyeiba shuka yake (Safwaan). Safwaan alimuombea yule mwizi asikatwe. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia: ‘Ungalifanya hivyo kabla ya kumleta kwangu).” [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na akaisahihisha Ibn Al-Jaaruwd na Al-Haakim]
1062.
وَعَنْ جَابِرٍ قَالَ: جِيءَ بِسَارِقٍ إِلَى اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فَقَالَ: {"اُقْتُلُوهُ". فَقَالُوا يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنَّمَا سَرَقَ. قَالَ: "اِقْطَعُوهُ" فَقَطَعَ، ثُمَّ جِيءَ بِهِ اَلثَّانِيَةِ، فَقَالَ "اُقْتُلُوهُ" فَذَكَرَ مِثْلَهُ، ثُمَّ جِيءَ بِهِ اَلرَّابِعَةِ كَذَلِكَ، ثُمَّ جِيءَ بِهِ اَلْخَامِسَةِ فَقَالَ: "اُقْتُلُوهُ"} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنِّسَائِيُّ، وَاسْتَنْكَرَهُ
وَأَخْرُجَ مِنْ حَدِيثِ اَلْحَارِثِ بْنِ حَاطِبٍ نَحْوَهُ. وَذَكَرَ اَلشَّافِعِيُّ أَنَّ اَلْقَتْلَ فِي اَلْخَامِسَةِ مَنْسُوخٌ
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliletewa mwizi akasema: ‘Muuweni’. Maswahaba wakasema: Ee Rasuli wa Allaah! Ameiba. Akasema: ‘Mkateni (mkono)’ akakatwa mkono, kisha akaletwa mara ya pili akasema: ‘Muuweni’. Akataja mfano wake. Kisha akaletwa mara ya tatu. Akaeleza kama alivyotangulia. Kisha akaletwa mara ya nne. Akataja mfano wake. Alipoletwa mara ya tano, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: ‘Muuweni’.”[10] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy na amesema ni Munkar]
An-Nasaaiy alipokea mfano wake kutoka kwa Al-Haarith bin Haatwib.[11] Ash-Shaafi’iy amesema kuwa kuuwawa kwa mara ya tano kumefutwa (mansuwkh)
[1] Kuna rai tofauti miongoni mwa ‘Ulamaa kuhusu kiasi cha thamani ya kitu kilichoibiwa ili mkono wa mwizi ukatwe. Tukisoma Ahaadiyth mbali mbali na maelezo ya ‘Ulamaa mbali mbali kinathibitisha kuwa wizi wa bidhaa zenye thamani chini ya moja ya nne ya dinari (ambayo ni sawa na dirhamu 3 wakati wa Maswahaba wa Nabiy) haihalalishi mkono wa mwizi ule kukatwa. Robo dinari ni chini ya gramu moja na nusu ya dhahabu.
[2] Hadiyth ikamalizikia: “Ikateremka Aayah:
إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّـهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا أُولَـٰئِكَ لَا خَلَاقَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيْهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٧﴾
“Hakika wale wanaobadilisha ahadi ya Allaah na viapo vyao kwa thamani ndogo; hao hawana sehemu yoyote katika Aakhirah na wala Allaah Hatowasemesha na wala Hatowatazama Siku Ya Qiyaamah na wala Hatowatakasa na watapata adhabu iumizayo” [Aal-‘Imraan: 77]
[3] Tukio hili lilitokea kwa bibi mmoja aitwae Faatwimah bint Aswad Makhzuwmiyah, ambae ni mwanamama kutoka katika familia kubwa inayoheshimika aliyeiba. Ilipotajwa hukumu ya kumkata mkono, watu wakaanza kutafuta wa kumuombea msamaha. Usaamah alionekana wa kutumika kumuombea. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitoa khutbah kali ambayo baadhi yake ipo katika hadiyth hii. Kishariy’ah mtu aliyeibiwa ana haki ya kumsamehe mwizi wake kabla ya jambo lile kupelekwa mahakamani. Hata hivyo kesi ikishapelekwa mahakamani hakuna njia ya kumsamehe tena mhusika. Mkono wake ni lazima ukatwe, na kumuombea kwa wakati huu haina maana kwani hairuhusiwi.
[4] Yaani wote watakuwa ni wamiliki wa mnyama huyo.
[5] Wizi wa kutumia silaha, ubadhirifu wa mali na udanganyifu haviingii katika adhabu ya kukata mkono. Udanganyifu unakusudia mtu aliyepatiwa amana kwa kuilinda anaitumia na kuondoka na mali ile huku akionesha sura nyingine. Ama wizi kwa njia ya ujambazi ni kuchukua mali ya mtu kwa nguvu na kwa uwazi kabisa. Ubadhirifu ni kutumia mali ya mtu mwingine vibaya kwa kutokuwepo kwake. Hata hivyo, ikiwa mtu ataazima kitu kwa mtu na mwisho akakana kuwa hajaazima, mtu huyu atachukuliwa kama ni mwizi na atakatwa mkono.
[6] Kuiba matunda hailazimishi mtu kukatwa mkono maadamu katika shamba lile hakukuwa na ukuta uliyozungushiwa. Likiwa shamba au bustani lenyewe lina ukuta uliozungushwa basi atawajibika na adhabu ile. Hivyo, msafiri ambae ameshaanza kupewa chakula na watu wa mji anaruhusiwa kula katika bustani iliyo na matunda pembezoni mwa ukuta.
[7] Ni Swahaba kutoka Al-Hijaaz ambae amepokea Hadiyth moja tu. Hammaad bin Salamah anamuelezea: “Alikuwa ni katika ukoo wa Al-Makhzuwm” wakati wa Humam bin Yahya amesema: ‘Alikuwa ni Answaar’
[8] Hadiyth hii inaelezea mambo mawili yaliyozingatiwa katika kutoa hukumu ya adhabu ya mwizi. Kwanza mali ya wizi ikombolewe kutoka kwake, au mwenyewe kukiri kuhusu hilo, siyo lazima kukiri mara mbili, mara moja inatosha kumuingiza hatiani na hukumu kutekelezwa kwake. Kuna tofauti ya rai ikiwa ushahidi unahitajika katika suala la wizi unapotokea. Kwa maneno mengine ni kuwa ikiwa mtuhumiwa hajakiri kuiba na hakuna kidhibiti kilichopatikana kwake na mashahidi wakapatikana kuwa ndie aliyeiba. Hukumu ya kesi kama hiyo siyo katika makubaliano ya ‘Ulamaa. Baada ya mkono kukatwa mafuta ya moto humwagwa ili kuzuia kutoka kwa damu. Ikiwa katika hali kama hii damu ikaendelea kumiminika na mtu akafa, kwa ajili hiyo ni jukumu la Hazina ya dola (Baytul-Maal) kulipa fidia kwa warithi wa aliyefariki.
[9] Ikiwa vitu vilivyoibwa vitapatikana kwa mwizi, vitarejeshwa kwa mwenyewe na mkono wa mwizi utakatwa kwa makubaliano ya ‘Ulamaa. Katika hali ya vitu vilivyoibwa kuharibika, hapa kuna tofauti ya rai kwa ‘Ulamaa kama alipe faini au laa.
[10] ‘Ulamaa wengi wanaona kuwa njia iliyoelezwa ya kumkata mwizi mkono na mguu ni kuwa kwa mara ya kwanza akiiba atakatwa kiganja cha mkono wa kuume. Kwa mara ya pili atakatwa fundo la mguu wa kushoto, mara ya tatu kiganja cha mkono wa kushoto na mara ya nne ni kifundo cha mguu wa kushoto.
[11] Huyu alikuwa Jumahi, Mqurayshi aliyezaliwa Ethiopia. Alikuwa gavana wa Makkah mwaka wa 66 Hijriyyah wakati wa ‘Abdullaah bin Az-Zubayr. Alimtumikia kwa muda wa miaka 6 na baada ya hapo akawa msimamizi wa Al-Masai wakati wa Marwaan alipokuwa gavana wa Madiynah wakati wa Mu’aawiyah.