01-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mwanamke Akitoharika Baada Ya Kuingia Alfajiri Afunge Au Itabidi Alipe Swawm?

 

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

01-Mwanamke Akitoharika Baada Ya Kuingia Alfajiri Afunge Au Itabidi Alipe Swawm?

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

 

Mwanamke akitoharika mara tu baada ya kuingia Alfajiri je atajizuia na kufunga siku hii? Au itabidi aje kulipa?

 

 

JIBU:

 

 

Mwanamke akitohariki baada kuchomoza Alfajiri,  ‘Ulamaa wana kauli mbili kuhusu kujizuia:

Kauli ya Kwanza:

 

Itabidi ajizuie siku ile nzima na asiihesabu siku ile bali itampasa ailipe, kauli hii ni mashuhuri kwa madhehebu ya Imaam Ahmad (Rahimahu-Allaah).

 

Kauli ya Pili:

 

Haimlazimu kujizuia siku ile nzima kwani ni siku ambayo hakuwajibika Swawm kwa kuwa kwake mwenye hedhi na sio katika wanaowajibishwa Swawm na kama ni hivyo basi hakuna faida kwake kujizuia. Na wakati huo sio wakati wa kuheshimika kwake kwani ni mwenye kuamrishwa kwa fitwrah mwanzo wa mchana na Swawm ya ki-Shariy’ah  ni kujizuia na vyenye kufunguza Swawm kwa ajili ya kumwabudu Allaah ('Azza wa Jalla)  tokea Alfajiri hadi kuzama kwa Jua.

 

Kauli hii ndio kauli iliyochukuliwa zaidi kuliko ile ya kulazimika kujizuia na kauli zote mbili atalazimika kulipa Swawm.

 

Share