14-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kutoka Damu Kwa Mwenye Mimba Mchana Wa Ramadhwaan Inaathiri Swawm Yake?
14-Kutoka Damu Kwa Mwenye Mimba Mchana Wa Ramadhwaan Inaathiri Swawm Yake?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Mwenye mimba anapotokwa na damu mchana wa Ramadhwaan je, Swawm yake inaathirika?
JIBU:
Damu ya hedhi ikitoka na akawa yuko katika Swawm basi Swawm yake itakuwa imeharibika kwa kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Je, kwani akiwa na hedhi si haswali na hafungi?”
Kwa hivyo tunachukuliwa kwa vinavyofunguza Swawm. Na kwa wenye nifaas ni vivyo hivyo, na kutoka damu ya hedhi na nifaas huharibu Swawm. Na kutoka damu kwa mwenye mimba mchana wa Ramadhwaan na ikiwa ni hedhi itakuwa ni hedhi kwa asiye na mimba yaani huathiri kwenye Swawm yake. Kama sio hedhi basi haiathiri.
Na hedhi ambayo inaweza kumpata mwenye mimba ni ile hedhi inakwenda ikirudi haijakatika tokea alipopata mimba bali ilikuwa ikimjia wakati wa ada yake. Hedhi hii kwa kauli iliyoungwa mkono zaidi ni huthibiti juu yake hukumu za hedhi. Ama damu ikikatika na baada ya muda akaona damu basi damu yenyewe sio damu ya ada yake basi hii haiathiri Swawm yake kwani sio damu ya hedhi.