15-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Akipata Damu Siku Moja Lakini Ya Pili Yake Hakuona Damu Afanyeje?
15-Akipata Damu Siku Moja Lakini Ya Pili Yake Hakuona Damu Afanyeje?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Pindi mwanamke akiona katika kipindi cha ada yake siku moja damu na siku nzima inayofuata haoni afanye nini?
JIBU:
Huu utohara au ukavu aliouona katika nyakati za hedhi yake haihesabiki kuwa ni utohara. Hapa yampata ajizuie kama anavyojizuia mwenye hedhi. Baadhi ya ‘Ulamaa wameserna: “Atakayeona damu na siku nyingine hakuna basi damu hiyo ni damu ya hedhi.”
Na huo usafi au utohara hadi ufikie siku kumi na tano na ikifika muda huo basi damu hiyo itakuwa ni Istihaadhwah na hili ndilo jambo mashuhuri kwa muono wa madhehebu ya Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu-Allaah).