17-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan Kwa Mwenye Hedhi Au Nifaas Akiangalia Mswahafuni
Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan Kwa Mwenye Hedhi Au Nifaas Akiangalia Mswahafuni
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Nini hukumu ya usomaji wa Qur-aan kwa mwenye hedhi na nifaas akiwa anaangalia Mswahafuni au anahifadhi na haswa tukizingatia katika hali ya dharura kuwa ni mwanafunzi au mwalimu?
JIBU:
Si vibaya kwa mwanamke mwenye hedhi na nifaas kusoma Qur-aan kwa haja kama vile yeye ni mwalimu au mwanafunzi ambaye anasoma uradi wake wa siku kama ni usiku au mchana. Ama usomaji wa Qur-aan kwa maana ya usomaji wa kupata ujira na thawabu asifanye kwa sababu ‘Ulaama wengi wanaona kuwa mwenye hedhi haimfali kusoma Qur-aan.