18-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Anawajibika Kubadilisha Nguo Baada Ya Kumaliza Hedhi Japokuwa Hazikuingia Damu?
Anawajibika Kubadilisha Nguo Baada Ya Kumaliza Hedhi Japokuwa Hazikuingia Damu?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Je inamlazimu kwa mwenye hedhi kubadilisha nguo zake baada ya kupata tohara pamoja na kujua kuwa nguo zenyewe hazijaingia damu wala najisi?
JIBU:
Haimpasi kufanya hivyo; kwa sababu hedhi hainajisi kiwili wili bali damu ya hedhi ndio ambayo hunajisi pale palipodondokea na ndio maana Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaamrisha wanawake nguo zao zikipata damu ya hedhi wakoshe kisha waswali nazo.