19-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hakuweza Kulipa Deni La Swiyaam Mpaka Imefikia Ramadhwaan Ya Tatu Kwa Sababu Ya Uzazi Kunyonyesha Na Ugonjwa Afanyeje?

Hakuweza Kulipa Deni La Swiyaam Mpaka Imefikia Ramadhwaan Ya Tatu

Kwa Sababu Ya  Uzazi Kunyonyesha Na Ugonjwa Afanyeje?

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

JIBU:

 

Anauliza muulizaji mmoja kuwa mwanamke amekula (hakufunga) siku saba katika Ramadhwaan akiwa ni mwenye nifaas, na hakulipa hata ikamjia Ramadhwaan nyingine na katika Ramadhwaan hii ya pili siku saba zikampita akiwa ananyonyesha  na hakulipa kwa hoja kuwa ana maradhi, afanye nini na inakaribia Ramadhwaan ya tatu kufika. Tupeni faida juu ya hilo na Allaah Atawalipeni?

 

 

JIBU:

 

Ikiwa mwanamke huyu kama alivyotaja mwenyewe kuwa ana maradhi na hawezi kulipa basi pindipo atakapoweza atafunga kwa kuwa ni mwenye udhuru hata kama itakuja Ramadhwaan nyingine. Ama kama hatokuwa na udhuru bali anajifanya kuwa ni mgonjwa na kufanya uvivu na kuzembea basi haifai kwake kuakhirisha kulipa Ramadhwaan hadi Ramadhwaan nyingine. ‘Aaishah (Radhwiya-Allaahu ‘anhaa) amesema: “Ilikuwa kwangu Swiyaam ambazo ninadaiwa sikuwa naweza kuzilipa isipokuwa mwezi wa Sha’baan.”

 

 

Kwa hili, ni juu ya mwanamke huyu ajiangalie mwenyewe kama hana udhuru basi atakuwa ni mkosaji na juu yake kutubia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  na afanye haraka kulipa kilicho katika dhima yake katika Swiyaa,. Ama kama ni mwenye udhuru hapana neno hata kama akichelewa mwaka au miaka miwili.

 

 

Share