20-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kuchelewa Kulipa Deni La Swiyaam Za Ramadhwaan
Kuchelewa Kulipa Deni La Swiyaam Za Ramadhwaan
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Baadhi ya wanawake inawajia Ramadhwaan ya pili ilhali wanadaiwa baadhi za Swiyaam katika Ramadhwaan ya kwanza. Wajibu wao ni nini?
JIBU:
Wajibu wao ni kutubia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa matendo haya kwani haifai kwa mwenye deni la Swiyaam za Ramadhwaan ya kwanza kuzichelewesha hadi Ramadhwaan ya pili bila ya udhuri kwa kauli ya ‘Aaishah “Nilikuwa nina deni la Swiyaam za Ramadhwaan na nilikuwa siwezi kuilipa hadi inapofika Sha’baan, ndipo nailipa.” Hii inathibitisha kwa dalili kuwa haiwezekani kuichelewesha hadi Ramadhwaan ya pili hivyo ni juu yake atubie kwa Allaah ('Azza wa Jalla) kwa alichokifanya na alipe siku alizowacha baada ya Ramadhwaan ya pili.