21-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Alikuwa Na Hedhi Saa Saba Mchana Na Hakuswali Adhuhuri Je Alipe Swalaah Hiyo?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
21-Alikuwa Na Hedhi Saa Saba Mchana Na Hakuswali Adhuhuri Je Alipe Swalaah Hiyo?
SWALI:
Mwanamke akiwa kwenye hedhi saa saba mchana kwa mfano naye hakuwa ameswali sala ya adhuhuri je anatakiwa kuilipa swala hiyo?
JIBU:
Katika hili kuna tofauti miongoni mwa ‘Ulamaa.
Kuna miongoni mwao waliosema: Haimpasi kulipa Swalaah hii; kwani hakupetuka mipaka au hakufanya uovu kwani inampasa yeye kuchelewesha Swalaah hadi mwisho wa wakati wake.
Na kuna miongoni mwao waliosema: Inampasa kulipa , yaani kulipa Swalaah ile kwa Hadiyth Ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) “Atakayediriki rakaa moja basi ameidiriki Swalaah.”
Na jambo la akiba ni kuilipa kwani ni Swalaah moja tu haina mashaka kuilipa.