22-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Akiona Damu Kabla Ya Kuzaa Siku Moja Au Mbili Je Aache Swawm Na Swalaah?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
22-Akiona Damu Kabla Ya Kuzaa Siku Moja Au Mbili Je Aache Swawm Na Swalaah?
SWALI:
Mwanamke mwenye mimba akiona damu kabla ya kuzaa kwa siku moja au mbili je kwa ajili hiyo ataacha kufunga na kuswali?
JIBU:
Pindi mwanamke mwenye mimba akiona damu kabla ya kujifungua kwa siku au siku mbili basi hayo ni maumivu ya kujifungua na hiyo ni damu ya Nifaas na aache Swalaah na Swawm.
Na kama akiwa hana maumivu hayo basi itakuwa ni damu chafu hakuna mazingatio ndani yake wala haimzuii na Swalaah na Swawm.