23-imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kutumia Vidonge Kuzuia Hedhi Ili Aweze Swiyaam Inafaa

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

 23-Kutumia Vidonge Kuzuia Hedhi Ili Aweze Swiyaam Inafaa?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Vipi kama nitatumia vidonge vya kuzuia kwenda mwezini ili nipate kufunga na watu?

 

 

 

JIBU:

 

 

Mimi natahadharisha hili, vidonge hivi vina madhara makubwa, hili lilinithibitikia kutoka kwa madaktari. Tutamwambia mwanamke “Jambo hili limeandikwa na Allaah ('Azza wa Jalla)  kwa banati wa wana Aadam, kwa hivyo kinai akichokuandikia Allaah ('Azza wa Jalla)  na funga pale ambapo hapana kizuizi, na ikitokea kizuizi fungua kuridhika na lile Alilokukadiria Allaah ('Azza wa Jalla).

 

Share