Pilau Ya Nyama Kondoo Na Mtindi
Pilau Ya Nyama Kondoo Na Mtindi
Vipimo:
Nyama iliyokatwa vipande - 1 Ratili (LB)
Mchele Basmati - 2 Magi
Chumvi ya wali - kiasi
Kitungu kilichokatwa katwa - 1 kikubwa
Kitunguu saumu (thomu/garlic) na tangawizi - 1 kijiko cha supu
Mtindi (yogurt) - ½ kikombe
Mchanganyiko wa bizari ya pilau ya tayari - 2 vijiko vya supu
Mafuta kidogo yakukaangia
Bizari manjano (haldi) - nusu kijiko
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha mchele na roweka nusu saa .
- Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown).
- Tia thomu na tangawizi na ukaange kidogo.
- Kisha weka bizari ya pilau halafu nyama huku unakaanga lakini nyama isigeuke rangi.
- Tia maji gilasi 1½ - 2 ichemke mpaka nyama iwive na karibu kukauka.
- Mimina mtindi na iachie moto mdogo ikauke kidogo.
- Kwenye sufuria nyingine chemsha mchele pamoja na chumvi na mafuta kidogo mpaka uive.
- Mimina wali juu ya nyama, kisha nyunyiza bizari ya manjano, kama vile wali wa biriani na ufunike kwa dakika kumi hivi.
- Changanya wali na nyama pamoja ikiwa tayari kuliwa kwa saladi.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)