Wali Wa Kukaanga Kwa Nyama Mbuzi Ilichomwa Ya Sosi Ya Ukwaju
Wali Wa Kukaanga Kwa Nyama Mbuzi Ilichomwa Ya Sosi Ya Ukwaju
Vipimo Vya Wali
Mchele Basmati - 4 vikombe
Vitunguu vya majani (Spring onions) - 5 miche
Pilipili mboga nyekundu (capsicum) - 1
Pilipili mboga manjano (capscimu) - 1
Nyanya kubwa - 1
Supu ya kidonge - 2
Siagi - 2 vijiko vya supu
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha mchele kisha roweka kiasi masaa matatu takriban.
- Katakata vitunguu majani, mapilipili boga, nyanya vipande kiasi.
- Weka siagi katika sufuria ya kupikia, weka katika moto iyayuke.
- Tia vitunguu majani, mapilipili boga, nyanya, kaanga kidogo tu.
- Tia mchele kaanga kidogo, kisha tia maji kiasi ya kuivisha mchele.
- Tia supu ya kidogo au supu yoyote, funika wali upikike moto. mdogodogo.
Vipimo Vya Nyama Mbuzi Na Sosi Ya Ukwaju
Nyama mbuzi mapande makubwa kiasi - 7/8 vipande
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Ukwaju mzito ulokamuliwa - 1 kikombe cha chai
Jiyra/cummin/bizari pilau - 1 kijiko cha chai
Nyanya kopo - 2 vijiko vya supu
Siki - 2 vijiko vya supu
Mafuta - ½ kikombe cha chai
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Changanya vitu vyote pamoja katika kibakuli kidogo.
- Weka nyama katika bakuli kubwa kisha tia mchanganyiko wa sosi, ubakishe sosi kiasi pembeni.
- Roweka kwa muda wa masaa 3 – 5
- Panga nyama katika bakuli au treya ya kuchomea katika oven.
- Pika (bake) kwa moto wa kiasi kwa muda wa saa takriban.
- Karibu na kuiva, epua, zidisha kuichangaya na sosi ilobaki.
- Rudisha katika jiko uendelee kuipika muda kidogo tu.
- Epua ikiwa tayari, weka juu ya wali uliopakuwa kisha mwagia sosi ya nyanya pilipili (chilii tomato sauce) ukipenda.