Wali Wa Nazi Wa Adesi, Bamia Na Mchuzi Wa Kamba
Wali Wa Nazi Wa Adesi, Bamia Na Mchuzi Wa Kamba
Vipimo
Mchele - 2 vikombe
Adesi -1 ½ vikombe
Nazi ya unga - 1 Kikombe
Maji (inategemea mchele) - 3
Chumvi - Kiasi
Vipimo Vya Bamia:
Bamia - ½ kilo
Vitunguu maji - 2 vya kiasi
Nyanya iliyosagwa - 1 kubwa
Nyanya ya kopo - 2 vijiko vya chai
Pilipili manga - ½ kijiko cha chai
Mafuta - 3 vijiko vya chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
Wali wa adesi
- Osha na roweka mchele na adesi .
- Chuja nazi kwa vikombe 3 vya maji tia chumvi kisha weka jikoni.
- Tui la nazi likishachemka tia mchele na adesi pamoja. Punguza moto, funika wali upikike kwa moto mdogo mpaka ukauke vizuri.
Bamia
- Katakata bamia vipande vya kiasi/ Katakakata vitunguu weka kando.
- Katika sufuria tia mafuta na kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi.
- Tia nyanya ilosagwa na nyanya ya kopo na pilipili manga na chumvi.
- Kisha Tia bamia punguza moto mdogo mdogo mpaka ziwive.
Vipimo: Mchuzi Wa Kamba
Kamba - 1Lb
Vitunguu vilokatwa katwa - 2
Nyanya ilokatwa katwa - 2
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chai
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 Kijiko cha chai
Bizari ya mchuzi (curry powder) - ½ Kijiko cha chai
Haldi – bizari ya manajano - ½ kijiko cha chai
Nyanya ya kopo - ½ Kijiko cha chai
Ndimu - 1
Chumvi - Kiasi
Mafuta ya kukaangia - 2 Vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Kaanga vitunguu kidogo hadi vilainike,
- Tia nyanya, thomu na piilipili mbichi. Endelea kukaanga, tia nyanya ya kopo, chumvi, bizari zote.
- Tia tia kamba na huku unakoroga mpaka wabadilike rangi na kuwiva. Kamulia ndimu na mchuzi uko tayari..