Mandi Na Nyama (Yemen)
Mandi Na Nyama (Yemen)
Vipimo
Mchele - 3 Magi
Nyama ya mafupa - 2 Ratili (LB)
Mafuta - ¼ kikombe
Vitunguu maji kata vikubwa vikubwa - 3 kikubwa
Bizari ya pilau ya unga (cumin) - 1 kijiko cha chakula
Pilipili manga - ½ kijicho cha chai
Hiliki - ½ kijiko cha chai
Karafuu ya unga - ¼ kijiko cha chai
Mdalasini nzima - 3 Vijiti
Mdalasini wa unga - ½ kijiko cha chai
Kitunguu saumu na tangawizi - 2 vijiko vya chakula
Nyanya iliyokatwakatwa - 1 nzima
Kidonge cha supu - 1 au 2
Zaafarani (ukipenda) roweka katika maji - 1 kijiko cha chai
Zabibu kavu (ukipenda) - ¼ kikombe
Pilipili mbichi - ukipenda
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Kwenye sufuria katakata nyama naisafishe vizuri kisha tia binzari zote pamoja na vitunguu viwili, nyanya freshi, thomu na tangawizi na chumvi kiasi acha ichemkie huku ukiongeza maji mpaka iwive vizuri.
- Ikishawiva epua nyama zote tia kwenye treya ya kuchomea kisha ukipenda unaweza kuongezea viungo au hivyohivyo ukaichoma (bake) kwa moto wa 350° C mpaka rangi ibadilike.
- Ile supu inayobaki ichuje vizuri weka kando kwa ajili ya kupikia wali.
- Tia mafuata katika sufuria, kisha kaanga tena kitunguu kimoja tia mdalasini kidogo na thomu na tangawizi na kidonge cha supu 1 au 2 acha ikaangike kisha mimina ile supu, ukipenda unaweza kutia rangi ya zafarani au rangi ya biriani acha ichemke kisia maji kutokana na mchele, kisha mimina mchele upike mpaka uwive.
- Ukishawiva pakua kwenye sahani kisha weka nyama yako juu ya wali tayari kwa kuliwa na saladi au pilipili.
Kidokezo:
Ukipenda unaweza kutia zabibu kavu kwenye wali.
Tolea na kachumbari yake.