Wali Wa Mboga Na Mchuzi Wa Kuku wa Tanduri
Wali Wa Mboga Na Mchuzi Wa Kuku wa Tanduri
Vipimo vya Wali:
Mchele basmati - 3 magi (kikombe kikubwa)
Mchanganyiko wa mboga za barafu
(Frozen vegetables) - 1 ½ mug
Chumvi - kiasi
Mafuta - 3 vijiko vya chakula
Kitungu maji (kilichokatwa) - 1
Bizari ya pilau (nzima) - 1 kijiko cha chakula
Namna Ya kutayarisha na kupika:
- Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
- Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 6.
- Tia chumvi.
- Yakisha kuchemka unatia mchele, chemsha usiive sana, uive nusu kiini. Mwaga maji na kuchuja wali.
- Unamimina Yale mafuta kwenye sufuria unakaanga bizari ya pilau kidogo na kitunguu kabla ya kugeuka rangi ya hudhurungi (brown).
- Tia mchanganyiko wa mboga za barafu.,
- Mimina wali, changanya vizuri, ufunike na uweke katika moto mdogo kwa dakika 20.
- Pakua tayari kwa kuliwa.
Vipimo Vya Mchuzi
Kuku - 2 Ratili (LB)
Chumvi - Kiasi
Mafuta - ¼ Kikombe
Nyanya Kata vipande - 4
Nyanya kopo - 2 vijiko wa chakula
Tangawizi - 1 kijiko ya chakula
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko ya chakula
Tanduri masala - 1 kijiko cha chakula
Kotmiri liliyokatwa - 3 vijiko vya chakula
Pilipili mbichi - 2
Pili masala - 1 kijiko cha chakula
Garam masala - ½ kijiko cha chakula
Bizari manjano - ½ kijiko cha chakula
Mtindi - 3 vijiko vya chakula
Pilipili boga (kata vipande virefu) - 1
Ndimu - 2 vijiko vya chakula
Namna ya kutayarisha na kupika:
- Kwenye bakuli tia kuku na changanya vitu vyote pamoja isipokua mafuta.
- Tia mafuta kwenye sufuria yakisha kupata moto mimina kuku umpike kwa muda ½ saa kwa moto kiasi.
- Pakua kuku kwenye bakuli au sahani na ukate vitunguu maji duara na umpambie. Tayari kwa kuliwa.