Makbuus Samak/ Makbuus ya Samaki (U.A.E)
Makbuus Samak/ Makbuus ya Samaki (U.A.E)
Vipimo
Mchele wa Basmati - 4 vikombe
Samaki wa chango - 2 Wakubwa
Vitunguu vilivyokatwakatwa - 3
Samli au mafuta - ¼ kikombe
Buharaat (bizari ya Makbuus) - 2 vijiko vya supu
Bizari ya manjano (haldi/tumeric) - 1 kijiko cha chai
Nyanya zikizomenywa na kukatwakatwa - 3
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 2 vijiko vya supu
Loomi (ndimu kavu) au ya unga - ½ au ½ kijiko cha chai
Mdalasini kijiti - 1
Karafuu nzima - 3
Hililiki nzima - 4
Maji - 5 vikombe
Kotmiri iliyokatwakatwa - ½ kikombe
Chumvi - kiasi
Baharaat – Bizari Ya Makbuus
Pilipili Manga - ½ kikombe
Gilgilani (Corriander seeds) - ¼ kikombe
Mdalasini vijiti - ¼ kikombe
Karafuu - ¼ kikombe
Bizari ya pilau (cumin seeds) - 1/3 kikombe
Hiliki- 2 vijiko vya chai
Paprika ya unga - ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Baharaat (bizari)
Chambua hiliki utoe kokwa zake, kisha tia vitu vyote katika mashine ya kusagia (grinder) usage hadi iwe unga.
Changanya na Paprika bizari ikiwa tayar.
Ihifadhi katika chupa yenye mfuniko wa kubana vizuri.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Makbuus
Vipimo Vya Samaki:
Kitunguu saumu(thomugalic) na tangawizi ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi ilosagwa - 2 vijiko vya supu
Pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai
Maji ya ndimu - 3 vijiko vya supu
Bizari ya mchuzi - 1 kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Samaki
- Changanya masala ya samaki katika kibakuli kisha mpake samaki vizuri na mwache kiasi robo saa akolee masala.
- Mchome (grill) samaki hadi aive huku ukimgeuza.
- Eupa weka kando.
Namna Ya kutayarisha Na Kupika Wali
- Osha na roweka mchele kwa muda kiasi.
- Katika sufuria ya kupikia, tia samli au mafuta, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Tia baharaat na bizari ya manjano, kaanga kwa dakika moja hivi.
- Tia nyanya, karafuu, loomi, mdalasini, hiliki, changanya vizuri na endelee kukaanga.
- Tia maji (inategemea mchele unaotumia, huenda ukahitaji zaidi)
- Mwaga mchele maji uliyorowekea, mimina mchele katika supu, tia kotmiri, changanya vizuri, funika uchemke mchele, punguza moto na pika wali kama inavyopikwa pilau ukoroge mara moja au mbili tu.
- Ukishaiva wali, pakua katika sinia/sahani na weka samaki juu ya wali.
Kidokezo:
- Ukipenda badala ya kupika wali katika sufuria baada ya kutia mchele na kukaribia kuiva, na kabla ya kukauka supu yote, mimina katika treya ya jalbosi (Treya ya foil) upike ndani ya oveni (bake) kwa mtoto wa takriban 400-450º kwa muda wa dakika 20-25.
- Baharaat hiyo inatumiwa katika vyakula vya nchi za Kiarabu (Gulf States), hivyo unaweza kutumia kupikia makbuus ya vitoweo vingine kama nyama na kuku na vyakula vinginevyo kama michuzi n.k.