Mahshi Waraqah ‘Anab - Majani Ya Zabibu Yaliyojazwa (Shaam)
Mahshi Waraqah ‘Anab - Majani Ya Zabibu Yaliyojazwa (Shaam)
Vipimo
Majani ya Zabibu (Grape leaves) - 1 Kilo
(au yanapatikana katika chupa)
Mchele wa Kimisri (Egyptian rice)
uliooshwa na kuchujwa - 2 Vikombe
(ni mchele wa chembe ndogo ndogo
zaidi kuliko wa kawaida)
Vitunguu maji vilivyosagwa - 5
Mafuta - ¼ kikombe
Kotmiri iliyokatwa ndogo ndogo kabisa - ¼ kikombe
Baqdunis (Parsely leaves) iliyokatwa
ndogo ndogo kabisa - ¼ kikombe
Nyanya ya kopo - ½ kibati
Ndimu ya maji - ½ kikombe
Mafuta ya zaituni (olive oil) - ½ kikombe
Viazi vilivyokatwa duara nyembamba - 3
Maji - 3 Vikombe
Bizari ya pilau ya unga (cumin powder) - ½ kijiko
Pilipili manga - ½ kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Kata vishina vya majani ya zabibu, kisha osha na uchemshe kidogo katika maji ya moto. Na ikiwa ni ya tayari katika chupa, yaoshe vizuri. kama mara tatu ukibadilisha maji ili kutoa chumvi yake, kisha yachemshe katika maji ya moto kwa muda mdogo tu kama dakika 5 kisha yachuje maji.
- Tia mafuta ¼ kikombe katika sufuria na kaanga vitunguu kidogo tu kisha epua.
- Tia mchele, nyanya ya kopo, pilipili manga, chumvi, bizari na uchanganye vizuri, kisha rudisha katika moto upike kama dakika 5 tu kisha epua.
- Tia kotmiri na Baqdunis uchanganye vizuri.
- Panga vipande vya viazi katika sufuria chini ili kuzuia kuganda majani ya zabibu.
- Fungua jani moja moja la zabibu utie mchanganyiko kisha ufunge kwa kukunja pande zote mbili kwanza ukiwa unafunika mchanganyiko, kisha zungurusha (Roll) na kukunja jani lote. Hakikisha unabana vizuri unapokujnga.
- Panga juu ya viazi kisha tia maji, ndimu ya maji, mafuta ya zaituni, kisha ufunike vizuri sufuria huku uweke kitu juu yake kizito ili maji yasiingie ndani ya sufuria wakati inachemka. (kama unavyopika pudini (pudding)
- Pika katika moto mkali kwanza kisha punguza na kuacha moto mdogo mdogo muda wa saa moja, kisha acha ipoe kidogo, fungua utoke mvuke.
- Pakua katika sahani ikiwa tayari.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)