Biriyani Ya Kababu

Biriyani Ya Kababu

 

 

Vipimo Vya Kababu

Nyama ya kusaga - 1 Kilo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa -1 kijiko cha supu

Vitunguu vilivyokatwa vidogo

vidogo (chopped) - 2

Kotmiri iliyokatwa ndogo ndogo

(chopped) - 1 kikombe

Chumvi - kiasi

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Bizari ya pilau (cumin powder) - 1 kijiko cha chai

Gilgilani iliyosagwa (Corriander powder)-1 kijiko cha chai

Mdalisini wa unga - ½ kijiko cha chai

Chenga za mikate (Bread crumbs) - 1 kikombe

Mayai - 2

 

Vipimo Vya Wali Na Masala

  1. Mchele (Basmati) - 5/6 Vikombe
  2. Vitunguu - 6 vya kiasi
  3. Mafuta - ½ kikombe 
  4. Nyanya zilizokatwa ndogo (chopped) - 4 kubwa
  5. Pilipili mboga ya kijani kata
  6. Ndogo ndogo - 2
  7. Pilipili mbichi nzima - 3
  8. Garam Masala - 1 Kijiko cha supu
  9. Hiliki ya unga - ½ kijiko cha chai
  10. Mtindi (Yoghurt) - ½ kikombe
  11. Nyanya ya kopo - 2 Vijiko vya supu
  12. Chumvi - kiasi
  13. Mafuta ya kunyunyzia katika wali - 3 vijiko vya supu
  14. Zaafarani au rangi za biriani
  15. ya manjano na kijani - kiasi.

 

Namna Ya Kutaarisha Na Kupima

Kababu

  1. Changanya nyama, na vitu vyote ispokuwa mayai na chenga za mkate .
  2. Tia mayai uliyoyapiga pamoja na chenga za mkate na changanya vizuri.
  3. Fanya madongo ya umbo la yai (oval) kisha panga katika treya ya oveni na uchome kababu katika oven.
  4. Epua zikiwa tayari na ziweke katika treya au bakuli utakalopikia biriani.

 

Masala 

  1. Tia mafuta katika sufuria na kaanga vitunguu hadi viwe vyekundu.
  2. Tia nyanya, pilipili mbichi, pilipili mboga, bizari zote, chumvi na kaanga kidogo.
  3. Tia nyanya ya kopo kisha tia mtindi, iache kidogo katika moto, kisha mimina juu ya kababu na uchanganye pamoja.
  4. Chemsha mchele uive nusu, tazama kiini kama kawaida, kisha chuja na umimine juu  ya masala.
  5. Tia rangi za biriani kama ni zaafarani au rangi ya manjano na kijani juu ya wali kidogo, nyunyizia mafuta kidogo na changanya kidogo tu juu  ya wali  .
  6. Funika kwa foil paper na pika katika oveni moto wa 450 Deg kwa muda wa dakika 20 hivi.
  7. Epua na pakuwa wali katika sahani kisha masala juu yake ikiwa tayari kuliwa.

 

Kidokezo:  Ni vizuri kutumia treya za oven za foil (Foil paper tray)

 

 

 

 

Share