Biriani Ya Nyama Ya Ng'ombe -2

Biriani Ya Nyama Ya Ng'ombe -2

 

Vipimo

Nyama - 2  Ratili (LB)

Chumvi - kiasi

Mafuta - 1 Kikombe

Samli - ½ Kikombe

Kitungu (Kata virefu virefu) - 3 Vikubwa                                                  

Nyanya  (kata vipande) - 2

Nyanya kopo - 1 Kijiko cha chakula

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 Kijiko cha chakula

Tangawazi - 1 Kijiko cha chakula

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1  Kijiko cha chai

Pilipili ya unga nyekundu - ½ Kijiko cha chai

Kotmiri   iliyokatwa - 2 Vijiko vya chakula

Viazi - 6

Gram masala - 1 Kijiko cha chai

Mtindi - ¼ Kikombe cha chai                                                 

 

Namna Ya kutaarisha Na Kupika

1.   Kwenya karai au (sufuria) mimina mafuta na samli.  Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Vitowe viweke pembeni.
2.   Kaanga viazi na viweke pembeni.
3.   Chukua sufuria tia nyama, thomu, tangawizi, pilipili, nyanya, nyanya ya kopo, mtindi,  na pilipili ya unga. Chemsha mpaka iive.
4.   Tia vile vitungu ulioyovikaanga, tia viazi, gram masala, kotmiri na yale mafuta uliokaangia vitunguu kama ¼ kikombe, acha moto mdogo mdogo kama ¼ saa, epua weka pembeni.
 
Vipimo Vya Wali
Mchele - 5 Magi (Kikombe kikubwa)
Hiliki nzima - 4
Mdalasini mzima - 1
Zafarani  -  ½  kijiko cha chai
Rangi ya biriani -  ¼  Kijiko cha
Mafuta yaliyokaangiwa vitunguu -  ½  Kikombe                                                      
Chumvi - kiasi                         
Roweka zafarani na rangi kwenye kikombe na ¼ kikombe  cha maji. Roweka kabla ya robo saa. 
 

Namna Ya Kutaarisha

  1. Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
  2. Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 10.
  3. Tia hiliki na mdalasini.
  4. Yakishachemka unatia mchele,chemsha usiive sana, unamwaga maji.
  5. Unamimina tena ule mchele ½ yake kwenye  sufuria, unatia rangi na zafrani kidogo, halafu unamimina
  6. mchele uliyobakia unatia rangi iliyobakia.
  7. Mafuta yake unayachemsha mpaka yachemke unamimina juu ya mchele, unarudisha motoni unaweka
  8. moto mdogo ukisha kuiva, tayari kupakuliwa.
  9. Unapakuwa wali unaweka chini kwenye sahani na juu yake sosi ya nyama.

 

 

Share