Pilau ya Nyama ya Kusaga Na Mboga Mchanganyiko
Pilau ya Nyama ya Kusaga na Mboga Mchanganyiko
Vipimo
Mchele - 2 Mugs
Viazi - 3
Nyama ya Kusaga - 1 Pound
Mboga mchanganyiko za barafu - 1 Mug (Frozen vegetable)
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 2 vijiko vya supu
Garam masala - 1 kijiko cha supu
Nyanya - 1
Kitungu maji - 1
Mdalasini nzima - 1 vijiti
Karafuu - 3 chembe
Pilipili mbichi - 1
Chumvi - kiasi
Maji - 2 ½ Mugs
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Mraba ya supu ya nyama - kidonge 1, au supu yenyewe kiasi cha kutia ladha (hakikisha supu isizidi kipimo).
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha mchele na uroweke kiasi kutegemea aina ya mchele.
- Katakata viazi kaanga katika mafuta, toa weka kando.
- Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
- Tia nyama ya kusaga, thomu na tangawizi, pilipili, bizari zote na chumvi. Kaanga hadi nyama iwive.
- Katakata nyanya uliyokatakata itie katika mchanganyiko wa nyama na endelea kukaanga kidogo tu.
- Tia mboga ya barafu (frozen vegetables)
- Tia maji, kidonge cha supu au supu ya nyama kiasi tu cha kutia ladha.
- Yatakapochemka tia mchele.
- Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.