Wali Wa Zaafarani Na Kuku Wa Kupaka
Wali Wa Zaafaraan Na Kuku Wa Kupaka
Vipimo
Wali:
Mchele - 3 Vikombe
Kitunguu kiichokatwa - 1
Pilipili boga nyekundu iliyokatwa vipande - 1
Mafuta - ¼ Kikombe
Zaafarani - 1 kijiko cha chai tia kwenye kikombe na maji robo roweka
Chumvi - 1 kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katika sufuria, tia mafuta, kaanga kitunguu mpaka kiwe kidogo rangu ya udongo (brown)
- Tia pili pili boga.
- Tia mchele, kaanga kwa muda wa dakika 3, tia zaafarani na chumvi.
- Tia supu uliyochemshia kuku iwe imoto.
- Pika wali katika moto mdogo hadi uwive.
Kuku
Kuku Mzima -1
Mayai ya kuchemsha - 6
Namna Ya Kupika Kuku
- Mchemshe kuku mzima na chumvi mpaka uhakikishe ameiva vizuri.
- Mtowe na muweke pembeni. Supu yake tumia katika wali kama ilivyo hapo juuu.
- Chemsha mayai, menya na kata vipande viwili kila yai moja weka kando
Vipimo Vya Sosi Ya Kuku Ya Nazi
Kitunguu - 1
Nyanya iliyokatwa vipande - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 1 kijiko cha supu
Garam Masala - ½ kijiko cha supu
Bizari ya manjano - ½ kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Pilipili masala ya unga - ½ kijiko cha chai
Nyanya ya kopo - 1 kijiko cha supu
Nazi ya unga - 1 kikombe
Maji ya ukwaju - ¼ kikombe cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Tia Mafuta vijiko 2 vya supu katika sufuria
- Kaanga kitunguu maji mpaka kiwe rangi ya udongo (brown).
- Tia thomu na tangawizi.
- Tia nyanya nzima iliyokatwa katwa.
- Tia garam masala, manjano, pilipili ya unga, nyanya ya kopo, kaanga vizuri.
- Changanya kwenye sufuria na ukwaju. Iache ichemke vizuri.
- Changanya nazi ya unga na maji vikombe viwili.
- Mtie kuku mpike vizuri na hilo tui.
- Mtie kwenye oveni kidogo.
Kupakuwa katika Sinia
- Pakuwa wali kwanza katika sinia
- Muweke kuku juu ya wali.
- Pambia mayai