Wali Wa Kukaanga Kwa Kidari Cha Kuku (Chicken Breast) Wa Kukausha
Wali Wa Kukaanga Kwa Kidari Cha Kuku
Vipimo vya Wali:
Mchele - 3 vikombe
*Maji ya kupikia - 5 vikombe
*Kidonge cha supu - 1
Samli - 2 vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Hiliki - 3 chembe
Bay leaf - 1
Vipimo Vya Kuku
Kidari (chicken breast) - 1Kilo
Kitunguu - 1
Tangawizi mbichi - ½ kipande
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7 chembe
Pilipili mbichi - 3
Ndimu - 2
Pilipilimanga - 1 kijiko cha chai
Mdalasini - ½ kijiko cha chai
Jira/Cummin ya unga - 1 kijiko cha chai
Maji - ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Wali:
- Osha na roweka mchele kisha weka sufuria katika moto tia samli ipashe moto.
- Tia hiliki, bay leaf, kaanga, kisha tia mchele ukaange kidogo.
- Tia maji, chumvi na kidonge cha supu, upike wali kama unavyopika pilau.
- *Maji kisia kwa kutegemea mchele ulivyo.
- *Unaweza kutumia supu yoyote badala ya kidonge.
Kuku:
- Katakata kidari cha kuku vipande vya kiasi, weka katika sufuria, tia ndimu, bizari zote, chumvi.
- Katakata kitunguu vipande vidogodogo, pilipili, na kitunguu thomu (chopped), tia katika kuku.
- Chuna tangawizi mbichi tia katika kuku. Changanya vitu vyote vizuri.
- Tia maji kiasi ¼ kikombe tu kiasi cha kumkaushia kuku. Weka katika moto mpike huku unageuzageuza. Anapokaribia kukauka epua akiwa tayari kuliwa na wali (na saladi upendayo)