Zurubiani (Wali Wa Ki-Saudia)
Zurubiani (Wali Wa Ki-Saudia)
Vipimo
Mchele - 5 mugs (kikombe kikubwa)
Nyama (au kuku) - 2 Ratili (LB)
Chumvi - Kiasi
Mafuta - 3/4 kikombe
Samli - 1/2 kikombe
Vitunguu Vikubwa (kata virefu virefu) - 6
Nyanya (iliyosagwa) - 6 vijiko vya chakula
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha chakula
Pilipili mbichi - ½ kijiko cha chai
Hiliki nzima - 6 chembe
Mdalasini nzima - 5 vijiti
Mtindi (yoghurt) - ½ kikombe cha chai
Karoti - 1
Mapilipili makubwa - 2 kijani na jekundu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Sosi
- Kwenye sufuria mimina mafuta na samli. Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown)
- Mimina nyama, abdalasini, hiliki na chumvi kwenye hiyo sufuria ya vitunguu ikaange moto wa kiasi mpaka nyama iwive.
- Saga ile Karoti pamoja na mtindi kwenye blender (mashine yakusagia) kisha imimine kwenye nyama
- Tia nyanya iliyosagwa.
- Ikichemka weka moto mdogo mdogo mpaka mafuta yake yaje juu.
- Tia zile pilipili ulizo zikata kata rangi mbili.
- Yatowe mafuta yote weka pembeni.
- Acha sosi pee yake.
Wali:
- Osha mchele uroweke kwenye maji kwa muda wa dakika 20
- Chemsha maji kwenye sufuria kiasi cha magi 10
- Yakishachemka unatia mchele, chemsha usiive sana, unamwaga maji.
- Unamimina ule mchele juu ya lile rojo (sosi)
- Mafuta uliyoyatoa kwenye sosi yapashe moto halafu unayamimina juu ya mchele, unarudisha motoni. Unaweka motot mdogo mdogo ukisha kuiva, tayari kupakuliwa.
- Unapakuwa wali unaweka chini kwenye sahani na juu yake sosi ya nyama.