Wali Wa Hudhurungi Na Kabeji
Wali Wa Hudhurungi Na Kabeji
VIPIMO VYA WALI
Mchele wa hudhurungi (brown rice)
na (wild rice kidogo ukipenda)Osha na Roweka - 2 Vikombe
Kitungu maji - 1 Kiasi
Kitunguu saumu - 1 Kijiko cha supu
Bizari ya manjano - 1/2 Kijiko cha chai
Mdalasini nzima - 1 kijiti
Iliki iliyosagwa - 1/4 Kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Pilipili manga - 1/4 Kijiko cha cha
Mafuta - 2 Vijiko vya supu
Majani ya Bay(bay leaves) - 1
Mbegu ya giligilani iliyoponwa (coriander seeds) - 1 Kijiko cha chai
Supu ya kuku ya vidonge - 1
Maji ya wali - 4 vikombe
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
- Kaanga kitungu, kabla ya kugeuka rangi tia thomu.
- Kisha weka bizari zote na ukaange kidogo.
- Tia mchele kisha maji na ufunike upike katika moto mdogo.
- Na ikishawiva itakuwa tayari kwa kuliwa na kabeji na kuku wa tanduuri.
VIPIMO VYA KABEJI
Kabeji iliyokatwa katwa - 1/2
Karoti iliyokwaruzwa - 1-2
Pilipili mboga kubwa - 1
Figili mwitu (celery) iliyokatwa - 1 au 2 miche
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu
Pilipili mbichi - 1
Kisibiti (caraway seed) - 1/4 Kijiko cha chai
Bizari ya manjano ya unga = 1/2 Kijiko cha chai
Giligani ya unga - 1 Kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Kitungu maji kilichokatwa -1
Kotmiri - upendavyo
Mafuta ya kukaangia - Kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
- Kwenye sufuria kaanga kitungu, figili mwitu kisha tia thomu na pilipili zote.
- Halafu tia bizari zote na ukaange kidogo.
- Kisha weka kabeji na chumvi, ufunike moto mdogo ilainike kidogo na sio sana
- Tia karoti na usiwache motoni sana, kisha zima moto na inyunyizie kotmiri juu.