Biriani Ya Kuku Wa Kuoka (Baked) Kwa Sosi Ya Zaafarani Na Rosi
Biriani Ya Kuku Wa Kuoka (Baked) Kwa Sosi Ya Zaafarani Na Rosi
Vipimo
Mchele ulionyooka (basmati/pishori) – Vikombe 3
Kuku – 1
Vitunguu – 5
Nyanya 3
Majani ya bay (bay leaves) kiasi mawili
Bizari ya biriani – kijiko cha supu.
Hiliki nzima chembe 5
Bizari ya manjano (haldi/turmeric) 1 kijiko cha chai
Pilipili nyekundu ya unga – kijiko 1 cha chai
Chumvi kiasi
Mafuta kiasi
Zaafarani – kijiko 1 kimoja
Arki (rose water)
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Roweka mchele kiasi ya nusu saa au saa moja kulingana na aina ya mchele.
- Muoshe kuku mkatekate vipande saizi upendayo. Usimtoe ngozi.
- Mchepushe kuku kwa viungo upendavyo kama chumvi, siki, tangawizi mbichi na thomu na ndimu. Kisha mwache muda kiasi.
- Muoke (bake) kuku katika oveni mpaka awive. Mtoe mweke kando. Atakuwa ametoa supu yake kiasi, imimine katika kibakuli.
- Weka mafuta kiasi, tia bay leaves, kaanga kidogo kisha tia vitunguu ukaange mpaka vigeuke rangi iwe ya hudhurungi (golden borwn).
- Katakata nyanya vipande vikubwa kiasi na ukaange kidogo. Tia bizari zote.
- Mimina supu kiasi iliyotoka katika kumuoka kuku, kiasi ya nusu kikombe. Changanya vizuri.
- Mtie kuku umchganye vizuri na masala. Weka kando masala.
- Chemsha mchele ukishaiva nusu kiini mwaga maji.
- Changanya zaafarani na maji ya rosy kisha nyunyizia katika mchele pale unapomimina mchele juu ya sosi ya biriani.
- Funika uweke katika moto mdogo mdogo mpaka mchele uive.
- Pakua katika sahani masala yakiwa juu ya wali.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)