Wali Wa Tambi Na Kuku Wa Sosi Ya Mtindi
Wali Wa Tambi Na Kuku Wa Sosi Ya Mtindi
Vipimo Vya Wali
Mchele - 3 vikombe
Tambi - 2 vikombe
Mafuta - ¼ kikombe
Chumvi
Vipimo Vya Kuku
Kuku kidari (boneless) aliyekatwa katwa vipande - 1 Kilo
Kitunguu maji kilichokatwa katwa - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Paprika - 1 kijiko cha supu
Masala ya kuku (tanduri au yoyote) - 1 kijiko cha supu
Ndimu - 2 vijiko vya supu
Mtindi (yoghurt) au malai (cream) - 1 kikombe
Mafuta - ¼ kikombe
Majani ya kotmiri (coriander) - ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali:
- Osha Mchele, uroweke.
- Tia mafuta katika sufuria, kaanga tambi zilizokatwakatwa hadi zigeuke rangi kuwa nyekundu.
- Tia mchele endelea kukaanga kidogo.
- Tia maji kiasi cha wali kupikika kama unavyopika pilau. Kiasi cha maji kinategemea aina ya mchele
- Funika katika moto mdogo mdogo hadi uive ukiwa tayari.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku
- Katika bakuli, changanya vitu vyote isipokuwa mtindi na kitunguu.
- Tia mafuta katika karai, kisha tia kitunguu ukaange muda mdogo tu, usikiache kugeuka rangi.
- Tia kuku na masala yake, endelea kukaanga, kisha tia mtindi au malai ufunike apikike na kuiva vizuri.
- Nyunyuzia kotmiri iliyokatwakatwa ikiwa tayari kuliwa na wali wa tambi.