Biriani Ya Nyama Mbuzi Ya Mtindi Na Zaafaraan
Biriani Ya Nyama Mbuzi Ya Mtindi Na Zaafaraan
Vipimo - Nyama
Nyama mbuzi - 1 kilo
Kitunguu menya katakata - 1
Nyanya/tungule - 2
Thomu (kitunguu saumu/garlic) saga - 5 chembe
Tangawizi mbichi – kuna/grate au saga - 1 kipande
Pilipili mbichi saga - 2
Bizari ya pilau nzima (cumin seeds) - ½ kikombe cha kahawa
Mdalasini - 1 kijiti
Karafuu nzima - 5 chembe
Gilgilani/dania (coriander seeds) - ½ kikombe cha kahawa
Bizari ya mchuzi - 1 Kijiko cha supi
Chumvi - Kiasi
Mtindi - 1 glass
Hiliki ilopondwa - 2 vijiko vya chai
Vitunguu – menya katakata slices kwa ajili ya kukaanga- 7- 9
Mafuta - Kiasi ya kukaangai vitunguu
Vipimo - Wali
Mchele wa pishori/basmati - 4 glass
Zaafarani roweka katika kikombe cha kahawa - Kiasi
Mafuta - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Katika sufuria, changanya nyama pamoja, kitunguu kimoja, tangawizi, thomu, nyanya, na viungo vyake isipokuwa mtindi, hiliki na vitunguu vilobakia.
Tia maji kisha funika ichemke mpaka iwive nyama na ikauke supu.
Tia mtindi na hiliki changanya pamoja.
Weka mafuta katika karai, kaanga vitunguu mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Toa uchuje mafuta. Kisha viponde ponde kwa mkono uchanganye na nyama.
Chemsha mchele uive nusu kiini, mwaga maji.
Mimina katika nyama utie zaafarani, funika upike wali hadi uwive.
Epua ukiwa tayari.
Bis-swihhah wal-hanaa (kunywa kwa siha na kufurahika)