Wali Wa Sosi Ya Samaki Tuna Na Viazi
Wali Wa Sosi Ya Samaki Tuna Na Viazi
Vipimo:
Sosi Ya Tuna
Tuna (samaki/jodari) - 2 Vikopo
Vitunguu (kata kata) - 3
Nyanya katakata - 3
Viazi (vilivyokatwa vipande vidogo - cubes) - 4
Mchanganyiko wa bizari - 1 kijiko cha supu
Chumvi - kiasi
Kidonge cha supu – 1
Wali:
Mchele - 3 Vikombe vikubwa (Mugs)
Mdalasini - 1 kijiti
Karafuu - chembe 5
Zaafarani kiasi roweka
Chumvi kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Kosha mchele roweka kidogo.
- Kaanga viazi hadi viwive, epua chuja mafuta.
- Kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi (brown).
- Tia nyanya kaanga, kisha tia bizari ukaange kidogo.
- Weka kidonge cha supu katika kibakuli kidogo tia maji ya moto kikombe kidogo cha kahawa uchanganye.
- Changanya supu katika sosi ulokaanga.
- Tia viazi changanya, Pamoja na vipande vya samaki tuna.
- Chemsha mchele pamoja na mdalasini na karafuu.
- Karibu na kuwiva, chuja maji kisha mwagia katika sosi ya tuna.
- Nyunyizia zaafarani kisha funika upike moto mdogo mdogo kama unavyopika biriani.
- Pakua katika sahani ulie kwa saladi upendayo
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)