Pilau Ya Nafaka Na Nyama Ya Kusaga
Pilau Ya Nafaka Ya Nyama Ya Kusaga
VIPIMO
Mchele - 3 vikombe
Nyama ya kusaga - 1 LB
Mchanganyiko wa Nafaka upendazo; maharagwe, njegere, mbaazi n.k 1 mug
Vitunguu maji kata vipande vipande - 3 vya kiasi
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - 2 vijiko vya supu
Mafuta - ½ Kikombe
Mchanganyiko wa bizari (Garam Masala) - 2 vijiko vya chai
Mraba ya supu ya nyama - vidonge 2, au supu yenyewe kiasi cha kutia ladha (hakikisha supu isizidi kipimo kwa kupunguza kipimo cha maji).
Maji (inategemea mchele) - 5
Chumvi - Kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
- Osha mchele na roweka.
- Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitunguu mpaka viwe brown.
- Tia Thomu na tangawizi, kaanga kidogo.
- Weka nyama ya kusaga, chumvi na garam masala, endelea kukaanga mpaka nyama iwive.
- Mwaga maji yaliomo katika kopo la nafaka na utie nafaka pekee humo.
- Tia maji na vipande vya supu (Maggi cubes) huku unavivuruga, koroga kidogo.
- Tia mchele, koroga kidogo.
- Funika na pika kwa moto mdogo mpaka karibu na kukauka ukikorogoka kidogo. (kama unavyopika pilau ya kawaida)
- *Epua uipike katika moto wa oven 350-400 Deg kwa muda wa dakika 15.
- *Kama sufuria uliyotumia sio ya kupikia katika oven, mimina katika chombo chochote kinachotumika kwa oven kama bakuli la pyrex au treya za foil.
- Pakua katika sahani na iko tayari kuliwa.