Wali Wa Dengu Kwa Samaki Wa Kukaanga
Wali Wa Dengu Kwa Samaki Wa Kukaanga
Vipimo
Mchele wa basmati - 3 Vikombe
Dengu - 2 vikombe
Viazi - 3 vikubwa
Kitunguu - 2 kubwa
Nyanya - 2
Pilipili mbichi kubwa - 3
Pilipilimanga - ½ kijiko cha chai
Garama Masala (bizari mchanganyiko) -1 kijiko cha chai
Supu ya vidonge (stock cubes) - 2 vidonge
Chumvi - kiasi
Mafuta - ¼ kikombe
Zaafarani - 1 kijiko cha chai
Samaki wa kukaanga
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Dengu kama sio za tayari kwenye kopo, roweka na zichemshe hadi ziwive
Masala Ya Dengu:
- Zaafarani – iroweke katika maji ya dafu dafu (warm) ya chini ya robo kikombe weka kando.
- Osha mchele, roweka.
- Menya viazi na vitunguu, katakata vitunguu, na nyanya , weka kando.
- Katakata viazi vipande vidogo vidogo kwa umbo la mchemraba (cubes).
- Katika sufuria tia mafuta yakipata moto, tia viazi ukaange kidogo kwa moto mdogo mdogo hadi kukaribia kuwiva, toa weka kando.
- Kaanga vitunguu hadi vigeuka rangi ya hudhurungi isiyokoza (light brown) kisha tia nyanya ukaange kidogo.
- Tia vidonge vya supu (stock cubes) uvivuruge katika mchanganyiko, katakata pilipili mbichi kwa urefu tia, uendelee kukakaanga. Tia bizari, chumvi.
- Zima moto, changanya dengu na viazi katika mchanganyiko huo.
Wali:
- Chemsha mchele kama kawaida ya kupika wali mweupe, kiini kiwe kimewiva nusu yake.
- Chuja maji kisha changanya katika mchanganyiko wa dengu.
- Nyunyizia zaafarani, uchanganye wali na mchanganyiko kidogo tu.
- Funika acha uive katika mtoto mdogo mdogo au tia katika oveni hadi uive kama kawaida ya kupika wali.
- Pakua katiha sahani na tolea na samaki yoyote wa kukaanga.
Kidokezo:
Ukipenda punguza mchanganyiko wa dengu kama vijiko viwili vya supu kwa ajili ya kujaza katika samaki.