Wali Wa Karoti Na Kuku Wa Kukaanga
Wali Wa Karoti Na Kuku Wa Kukaanga
Vipimo Vya Wali
Mchele wa Basmati/Pishori - 1 kilo moja
Vitunguu maji - 3
Karoti - 2
Siagi - 3 vijiko vya supu
Kidonge cha supu (stock) - 1 kimoja
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Ósha mchele uroweke kama saa moja au mbili
- Katakata vitunguu vipande vidogodogo (chopped) weka kando.
- Kwaruza karoti (grate) weka kando.
- Tia siagi katika sufuria ya kupikia wali, weka katika moto iyayuke
- Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kiasi tu.
- Tia maji kiasi ya kupikia wali, changanya na kidonge cha supu.
- Yakichemka tia mchele, koroga, funika uweke moto mdogo mdogo.
- Kabla ya maji kukauka tia karoti changanya wali kisha funika uive kama unavyopika pilau.
Vipimo Vya Kuku Wa Kukaanga
Kuku alokatwakatwa - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa - 2 vijiko vya supu
Bizari ya mchanganyiko/garam masala - kijiko cha supu
Mtindi/Yoghurt - 1 kijiko cha supu
Ndimu - 1
Chumvi - kiasi
Mafuta ya kukaangia - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Ukishamuosha kuku, mchuje atoke maji yote.
- Changanya viungo vyote katika kibakuli kidogo.
- Changanya pamoja na kuku kisha acha akolee viungo (marinate) kwa muda wa masaa mawili takriban.
- Weka mafuta katika karai na kaanga kuku, akiwiva yu tayari kuliwa na wali.