Pilau Ya Nyama Ng'ombe Karoti Na Zabibu (Afghanistan)
Pilau Ya Nyama Karoti Na Zabibu
Vipimo - Nyama
Nyama ng’ombe ya mifupa ilokatwa vipande - 1 kilo
Tangawizi na thomu (somu/garlic) ilosagwa - 2 vijiko vya supu
Bizari mchanganyiko/garama masala - 1 kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Vipimo - Wali
Mchele - 4 glass
Mbatata/viazi menya katakata - 3 kubwa
Vitunguu katakata - 5
Kitunguu thomu kilosagwa (garlic/somu) - 1 kijiko cha supu
Hiliki ya unga - 1 kijiko cha chai
Bizari nzima ya pilau/cumin - 1 mti
Samli au mafuta - 2 Vijiko vya supu
Karoti zilokatwakatwa nyembamba - 6-7
Zabibu - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katika sufuria weka mafuta kijiko kimoja cha supu tia nyama na viungo vyake.
- kaushe katika moto hadi ikaribie kukauka kisha tia maji kiasi cha kuivisha na kubakisha supu ya mchele.
- Katika sufuria ya kupikia weka samli au mafuta ishike moto.
- Tia mbatata/viazi kaanga, tia vitunguu kaanga kidogo.
- Tia kitunguu thomu, hiliki, bizari ya pilau endelea kukaanga hadi viwe rangi ya brown kidogo.
- Tia mchele kaanga kidogo, kisha mimina nyama na supu yake. Funika wali uwive.
- Weka kikaangio katika moto, tia samli kijiko kimoja kisha tia karoti na zabibu, kaanga kwa sekunde chache tu kwa ajili ya kulainisha karoti na zabibu.
- Utakapopakuwa wali, pambia juu karoti na zabibu.
Kidokezo: Pika nusu ya vipimo ikiwa ni familia ndogo.