Wali Wa Nyanya Wa Kukaanga
Wali Wa Nyanya Wa Kukaanga
Vipimo
Mchele basmati, pishori - 3 vikombe
Vitunguu katakata - 2
Nyanya/tungule katakata - 5 takriban
Viazi/mbatata menya katakata - 3 kiasi
Thomu (saumu/garlic) ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha kulia
Hiliki ya unga - ½ kijiko cha chai
Kidonge cha supu - 2
Chumvi - kisia
Mafuta - ½ kikombe
Maji ya moto au supu - 5 takriban
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha na roweka mchele
- Katika sufuria weka mafuta yashike moto, tia viazi, vitunguu ukaange.
- Vikianza tu kugeuka rangi tia thomu na bizari, hiliki, endelea kukaanga kidogo.
- Tia nyanya kaanga lakini usiache zikavurugika sana.
- Tia mchele ukaange chini ya dakika moja.
- Tia maji ya moto, na kidonge cha supu au supu yoyote kiasi cha kufunika mchele yazidi kidogo.
- Koroga vichanganyike vitu, kisha funika upike kama pilau.
- Pakua ikiwa tayari, tolea kwa samaki wa kukaanga au kitoweo chochote kile. Bonyeza kiungo kifuatacho:
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)