Skip to main content

Samaki Wa Changu Wa Kukaanga

Vitoweo

Samaki Wa Changu Wa Kukaanga

Vipimo 

Samaki changu - 3 wa kiasi

Bizari mchuzi - 2 vijiko cha supu

Pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai

Ndimu - 2 kamua

Chumvi - kisia

Mafuta ya kukaangia - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Osha samaki mchuje maji.
  2. Changanya bizari, chumvi, pilipili na ndimu.
  3. Mpakaze samaki vizuri kisha mwache muda akolee viungo.
  4. Kaanga katika mafuta ya moto ugeuze mpaka ageuka rangi,
  5. Weka katika sahani tolea kwa mhogo, ndizi mbichi, wali wa nyanya au upendavyo.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)