Pilau Ya Kuku Kwa Mchele Wa Mbeya
Pilau Ya Kuku Kwa Mchele Wa Mbeya
Vipimo
Mchele wa mbeya unaonukia - 1 kilo
Kuku - 1
Vitunguu - 3
Viazi/mbatata - 5
Jira/bizari ya pilau nzima - 3 vijiko vya supu
Mdalasini - 1 kijiti
Pilipili manga - 1 kijiko cha supu
Hiliki - 3 chembe
Karafuu - 5 chembe
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 3 vijiko vya supu
Tangawizi mbichi ilosagwa - 3 vijiko vya supu
Mafuta ya kupikia - ½ kikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu na tangawizi yote..
- Menya viazi, katakata vipande vya kiasi.
- Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau.
- Tia bizari zote isipokuwa hiliki.
- Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu thomu/somu ukaange kidogo.
- Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi.
- Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau.