Pilau Ya Kuku
Pilau Ya Kuku
Vipimo
Mchele wa basmati - 3 vikombe
Kuku - ½
Viazi - 4
Vitunguu - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 2 vijiko vya supu
Binzari ya pilau nzima - 1 Kijiko cha chakula
Binzari ya pilau - ½ kijiko cha chai
Pilipili manga nzima - ½ kijiko cha chai
Karafuu nzima - 8
Iliki nzima - 6
Mdalasini nzima - 5 vijiti
Pilipili mbichi iliyosagwa - 2
Chumvi - kiasi
Mafuta ya kupikia - ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
- Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele.
- Kata kuku vipande upendavyo, safisha kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu na tangawizi.
- Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria.
- Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi.
- Tia thomu na tangawizi na binzari zote kaanga kidogo
- Kisha tia viazi kanga kidogo kisha tia kisha tia vipande vyako vya kuku na supu acha ichemke kidogo kisha tia maji ukisie kutokana na mchele unaotumia.
- Mwisho tia mchele koroga uchanganye na vitu vyote acha ichemke kiasi kisha funika na punguza moto mpaka uive (huku ukiugeuzageuza)
- Ukishakuwa tayari pakua kwenye sahani tayari kwa kula na salad na pilipili.