Pilau Ya Nyama Ya Mbuzi Kwa Kachumbari Ya Asili
Pilau Ya Nyama Ya Mbuzi Kwa Kachumbari Ya Asili
Vipimo:
Mchele wa basmati - 3 vikombe
Nyama mbuzi – kilo 2
Viazi - 3
Vitunguu – 5 kata slices
Kitunguu saumu (thomu/garlic) iliyosagwa - 2 vijiko vya supu
Bizari ya pilau nzima (cumin seeds) – Vijiko 3 vya supu
Mdalasini – kijiti kimoja
Pilipili manga – chembe kiasi
Karafuu nzima – kiasi chembe 7
Hiliki nzima – kiasi chembe 7
Chumvi - kiasi
Mafuta ya kupikia - ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
- Osha mchele na roweka
- Changanya nyama na chumvi na tangawizi, kisha chemsha nyama kwa maji kiasi vikombe 6. Ikiwiva weka kando, na itabakia supu yake kiasi.
- Weka mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vikaribie kugeuka rangi.
- Tia vipande vya viazi ukaange kidogo.
- Tia bizari nzima, pilipili manga, karafuu, kijiti cha mdalasini.
- Vuruga hiliki kisha tia pamoja na thomu, uendelee kukaanga kidogo tu.
- Mimina mchele kaanga kidogo, kisha mimina nyama na supu yake, maji yawe kiasi ya vikombe 5.
- Koroga kisha funika upike pilau kwa moto mdogo wa kiasi hadi iwive.
- Pakua utolee kwa kachumbari ya asili.
Bonyeza Upate Pishi La Kachumbari Ya Asili:
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)