Ugali Kwa Mchuzi Wa Samaki Wa Kuchoma, Nyanya Mshumaa Za Kukaanga, Achari
Ugali Na Mchuzi Wa Samaki, Nyanya Mshumaa Za Kukaanga Na Achari
Vipimo Vya Ugali:
Unga wa mahindi - 4 vikombe
Maji - 6 kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Tia maji kiasi katika sufuria wacha yachemke hasa
- Tia unga kidogo kidogo huku ukikoroga mpaka ukamatane
- Punguza moto huku ukiendelea kuusonga
- Endelea kusonga kwa dakika kadhaa mpaka uanze kuchambuka
- Kisha mimina kwenye bakuli au sahani na itakuwa tayari
Vipimo Ya Upishi Wa Mchuzi Wa Samaki Wa Kuchoma Wa Nazi
Samaki:
Samaki wa Nguru - kiasi vipande 5 - 6
Pilipili mbichi - 3
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 5 chembe
Tangawizi mbichi - 1 kipande
Bizari ya samaki - 1 kijiko cha supu
Pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai
Ndimu - 3 kamua
Chumvi - kiasi
- Ukipenda mkate samaki vipande kiasi.
- Saga vipimo vyote vinginevyo katika mashine. Mchanganyiko ukiwa mzito ongezea ndimu
- Changanya pamoja na samaki upake vizuri vipande vya samaki
- Acha kwa muda wa nusu saa vikolee mchanganyiko
- Panga samaki katika treya ya kupikia ndani ya oveni, kisha mchome (grill) samaki huku ukigeuza hadi viwive.
- Epua weka kando.
Mchuzi:
Nyanya/tungule - 3
Kitunguu - 2
Bizari ya manjano/haldi - ¼ kijiko cha chai
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Tui la nazi zito - 3 vikombe
Chumvi - kiasi
- Katakata vitunguu na nyanya vidogodogo (chopped) weka kando
- Weka mafuta katika karai au sufuria, kaanga vitunguu hadi vianze kugeuka rangi
- Tia nyanya kaanga pamoja na tia bizari ya njano/haldi .
- Tia tui la nazi, chumvi koroga .
- Mwishowe tia vipande vya samaki na rojo lake litakalobakia katika treya, mchuzi uko tayari.
Upishi wa Mboga Ya Nyanya Mshumaa/Chungu unapatikana katika kiungo kifuatacho:
Nyanya Za Mshumaa/Chungu Za Kukaanga
Upishi wa Achari Tamu Na Kali Ya karoti Na Nyanya/Tungule unapatikana katika kiungo kifuatacho:
Achari Tamu Na Kali Ya Karoti Na Nyanya/Tungule