Biriyani Ya Nyama Ng'ombe - 1
Biriyani Ya Nyama Ng'ombe - 1
Vipimo Vya Masala
Nyama vipande - 3 LB
Mtindi - ½ kopo
Kitunguu (thomu/galic) - 1½ kijiko cha supu
Tangawizi - 1½ kijiko cha supu
Nyanya - 2
Pilipili mbichi - kiasi
Nyanya kopo - 4 vijiko vya supu
Vidonge supu - 2
Pilipili nyekundu paprika - kiasi
Bizari zote saga - 2 vijiko vya supu
Viazi - 4
Mafuta - 2 mug
Samli - ½ kikombe
Vitungu - 6
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Kwenye sufuria tia nyama, saga nyanya na thomu, pilipili mbichi, tangawizi. Mimina kwenye nyama na mtindi, tia na nyanya kopo, bizari paprika, vidonge vya supu, chumvi kisha changanya vyote pamoja weka motoni.
- Katika sufuria nyengine tia mafuta na samli kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi toa weka pembeni.
- Kanga viazi weka pembeni.
- Chukua mafuta kidogo uliyokangia tia kwenye nyama acha katika moto wa kiasi mpaka nyama iwive na maji ya punguke.
- Tia viazi na vitunguu vivunje vunje tia ndani ya nyama acha moto mdogo.
Vipimo Vya Wali
Mchele - 5 mug
Maji - kiasi
Chumvi - kiasi
Mafuta uliyokaanga vitungu - kiasi
Rangi ya biriani - ¼ kijiko cha chai
*Zafarani - ½ kijiko cha chai
*roweka rangi na zafarani
Namna Ya Kutarisha Na Kupika Wali
- Osha mchele roweka muda wa saa.
- Chemsha maji kama magi 10 hivi na chumvi tia mchele.
- Uache uchemke ukishaiva kiini nusu, mwaga maji chuja.
- Mimina juu ya nyama tia rangi na mafuta kwa juu funika.
- Aacha kidogo katika oveni kwa muda wa dakika 20 hivi kisha epua ikiwa tayari.