Viazi Vya Nazi Kwa Nyama
Viazi Vya Nazi Kwa Nyama
Vipimo
Viazi - 3lb
Nyama - 1lb
Kitunguu - 1
Nyanya - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha chai
Manjano - ½ kijiko cha chai
Curry powder - ½ kijiko chai
Nyanya kopo - 1 kijiko cha chai
Pilipili ya unga - kiasi upendavyo
Chumvi - kiasi
Kidonge cha supu - 1
Tui la nazi - 1 kopoau zaidi
Mtindi ukipenda - 3 vijiko vya supu
Kotmiri - kiasi ya kupambia
Nazi ya unga - 4 vijiko vya supu
Mafuta - 2 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Kata nyama vipande vipande kisha chemsha na chumvi mpaka iive.
- Menya maganda viazi na ukate slice kubwa weka pembeni
- Kata kata kitunguu kisha kaanga na mafuta mpaka vibadilike rangi
- Tia thomu, bizari ya manjano, pilipili ya unga, nyanya kopo
- Kata kata nyanya nzima vipande vidogo tia na kidonge cha supu.
- Kisha tia viazi, nyama na tui la nazi finika mpaka viazi viwive lakini visiwe vikavu.
- Tia mtindi na nazi ya unga kama vijiko 4 vya supu iache motoni kidogo kisha pakua, tupia kotmiri juu na itakuwa tayari kuliwa.